Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe ili kuzindua rasmi maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, leo Juni 03. 2012, yanayofanyika Kitaifa mkoani Kilimanjaro.
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Kikundi cha BEP-Environmental Initiatives Consortium, Jensen Siria, kuhusu matumizi na utengezaji wa majiko ya gharama nafuu, wakati alipotembelea katika Banda la kikundi hicho, katika maonesho ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, aliyoyazindua Kitaifa, leo Juni 03, 2012, Viwanja vya Mashujaa Mkoani Kilimanjaro.
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa Masoko wa Kundi la Mradi wa WASH, Kelvin Mwanshilo, wa Shirika la Care, kuhusu vyoo mbadala vya gharama nafuu, wakati alipotembelea katika Banda la kikundi hicho katika maonyesho ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, Viwanja vya Mashujaa Mkoani Kilimanjaro.
Kikundi cha ngoma za asili cha mkoani Kilimanjaro, kikitoa burudani wakati wa uzinduzi huo, viwanjani hapo leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa mkoani Kilimanjaro, wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, leo Juni 03, 2012, ambayo yanafanyika Kitaifa mkoani humo.
No comments:
Post a Comment