Ma afisa wa Nigeria wanasema kuwa ndege ya abiria imeanguka kwenye eneo la makaazi mengi, katika mji mkubwa kabisa wa nchi, Lagos.
Walioshuhudia tukio hilo wanasema waliona ndege ikigonga jengo na kuwaka moto.
Ndege ilikuwa imebeba kama mia-moja-na-50. Haijulikani wangapi wamenusurika.
Mkuu wa Idara inayoshughulika na safari za ndege, Harold Denuren, alisema ndege hiyo ilikuwa inatoka Lagos, kusini mwa Nigeria, kuelekea mji mkuu Abuja, kaskazini mwa nchi.
(Alisema ni ndege ya kampuni binafsi ya Dana Air)
Ndege hio ilianguka katika eneo lililo nje kidogo mwa uwanja wa ndege.Taarifa ilisema kua wataalamu wa dharura walikua njiani kufika mahali pa tukio.
Habari zinasema kua hali ya hewa ilikua shuari kukiwa na jua bila sababu ya kusababisha hitilafu.
Nigeria kama Mataifa mengi ya Kiafrika ina rekodi mbovu ya usalama wa safari za anga, ingawa juhudi kiasi zimefanywa katika kuboresha hali hio tangu kipindi cha janga la ajali za ndege mnamo mwaka 2005.
No comments:
Post a Comment