TANGAZO


Thursday, June 7, 2012

Changia Elimu Kata ya Kipawa, milioni 421.8 zapatikana


Mbunge wa Jimbo la Segerea, Dk. Makongoro Mahanga (kulia), Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (kushoto) na Mwenyeji wa harambee ya kuchangia mpango wa elimu wa Kata ya Kipawa, Diwani wa Kata  hiyo Bonah Kaluwa, wakimuongoza Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ambaye alikuwa mgeni rasmi kuingia ukumbini.

Mgeni rasmi katika harambe ya kuchangia Elimu Kata ya Kipawa, Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa (wa pili kulia), Mbunge wa Jimbo la Segerea, Dk. Makongoro Mahanga (kushoto), Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (kulia), Mwenyeji wa harambee hiyo, Diwani wa Kata  Kipawa Bonah Kaluwa (wa tatu kulia), Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita (wa tatu kushoto),  wakiwa wamesimama pamoja na wadau wengine kwenye harambe hiyo, jana usiku.
Baadhi ya wageni na wadau mbalimbali wakiwa kwenye harambee hiyo, ukumbini hapo.
.Diwani wa Kata ya Kipawa Bonah Kaluwa, akitoa neno la shukurani kabla ya kuanza kwa harambee hiyo.

Mgeni rasmi wa harambee hiyo, akimpa mkono wa asante mwakilishi wa Kampuni ya Home Shopping Centre, Madiha Al Harthy (kushoto), baada ya kuchangia sh. milioni 22.

Mkurugenzi wa SONGAS Limited, Christopher Ford (katikati), akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya dolla za kimarekani 10,000, mgeni rasmi wa harambee hiyo. Kushoto ni Meneja rasilimali Songas, Agatha Keenja.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Shinyanga, Hamisi Mgeja (katikati) akipongezwa na Mgeni rasmi wa harambe hiyo baada ya kuchangia sh. 500,000.

Diwani wa Kata ya Kipawa Bonah Kaluwa (katikati), akijadiliana jambo na Mgeni rasmi katika harambe hiyo, Edward Lowassa na Meya Silaa.

Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (kushoto), akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh.milioni 10, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, aliyekuwa mgeni rasmi katika harambee ya kuchangia mpango wa elimu Kata ya Kipawa, iliyofanyika Dar es Salaam jana usiku. Fedha hizo zilitolewa na Manispaa hiyo ambapo zaidi ya sh. milioni 400 zilipatikana. (Picha zote na Dotto Mwaibale)
Lowasa achangisha sh. milioni 421.8 harambe ya Changia Elimu Kipawa
Na Dotto Mwaibale
 Juni 7, 2012.
WAZIRI Mkuu wa zamani , Edward Lowassa, ameendelea kuwa mstari wa mbele katika harakati zake za kuchangisha fedha baada ya kuchangisha zaidi ya Sh.bilioni 421.8 kwa ajili ya kuboresha Mfuko wa Elimu Kata ya Kipawa katika Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaam.

Katika harambee hiyo iliyofanyika Hoteli ya Kilimanjaro Kempiski Dar es Salaam, Lowassa ambaye ni mbunge wa Monduli alichangia Sh.milioni 10.

Katika harambee hiyo miongoni mwa makampuni yaliyochangia kiasi kikubwa ni  Lion Club Sh.milioni 70, Home Shipping Center Sh.milioni 22, African Barrick Gold Dola 10,000, Songas Dola 10,000, Maersk Sea Line ilichangia Sh.Miliono 90, na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja alichangia milioni Sh.10.

Wengine waliochangia ni madiwani, viongozi wa Chama Cha Mapinduzi, Chadema, taasisi za watu binafsi na mtu mmoja mmoja ambapo Radio Clauds walitoa muda wa hewani wa kutangaza mpango huo wenye thamani ya sh. milioni 12.

Akizungumza kabla ya kuendesha harambee ya kuchangisha, aliwataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri kuendelea kuwahamasisha wananchi kuwekeza katika kuchangia sekta ya elimu.
Lowassa alimpongea Diwani wa Kata ya Kipawa, Bonnah Kaluwa, kwa jitihada zake alizozionyesha za kuchangia elimu na kuwataka madiwani wengine kuiga mfano huo.
Diwani wa Kata ya Kipawa,  Bonnah Kaluwa,  alisema shule saba za Msingi na Sekondari zilizopo kata hiyo zinakabiliwa na changamotonyingi  zikiwemo za upungufu wa vyumba vya madarasa hali inayosababisha wanafunzi kati ya 140 hadi 160 kusomea katika darasa moja huku wakiwa wamekaa chini.
“Shule nyingi katika kata yangu zinakabiliwa na changamoto nyingi, kwa mfano Shule ya Msingi ya Majani ya Chai ina vyumba vya madarasa nane wakati wanafunzi waliopo ni 2,200,  Shule ya Msingi ya Minazi Mirefu madarasa yake yaliyopo ni machakavu pia hayatoshelezi,”alisema Kaluwa.
Kaluwa alisema jitihada nyingine zilizofanywa katika kutafuta pesa kwa ajili ya kuziboresha shule hizo ambapo Machi 17 mwaka huu kuliitishwa matembezi ya hisani yaliyoongozwa na mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Aliongeza kuwa katika hafla hiyo kiasi cha shilingi milioni 15 kilichangwa na wadau mbalimbali ambapo kati ya hizo Sh.Milioni 3 zilitolewa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Clouds Media Group ambao walitoa shilingi milioni moja na wanafunzi kadhaa wa shule za msingi na sekondari.
Mbunge wa Jimbo la Segerea Dk.Makongoro Mahanga alisema katika jimbo hilo shule nyingi zinakabiliwa na changamoto nyingi hivyo alitoa mwito kwa wananchi na madiwani wa eneo hilo kuunga mkono jitihada za kuchangia elimu ili kuwaondolea wanafunzi adha wanayopata ya kukosa mazingira bora ya kuopata elimu.

No comments:

Post a Comment