Kiongozi mmoja wa kidini nchini Nigeria, mesema kuwa aonongoza mazungumzo ya upatanishi kati ya wapiganaji wa Boko Haram na serikali ya jimbo.
Sheikh Dahiru Bauchi amesema kuwa pande hizo mbili zimekubaliana kuanzisha mazungumzo juu ya namna ya kumaliza harakati za kundi hilo haramu.
Taarifa ya Sheikh Dahiru Bauchi inatokea wakati kukiwa na uhasama baina ya vikosi vya usalama nchini Nigeria na kundi la Boko Haram.
Tangu siku ya jumapili kumekuwepo na mashambulio mapya yanayofanywa na kundi hilo na vikosi vya usalama vinasema kua vimewaua wapiganaji 16 wa kundi hilo hapo jana jumanne.
Sheikh Dahiru ndiye kiongozi wa kundi la Kiislamu la Tijjaniyya mojawapo ya makundi makubwa ya Kiislamu nchini Nigeria.
Ingawa Boko Haram si sehemu ya kundi hilo, kiongozi huyo anaheshimiwa mno kama msomi katika dini ya Kiislamu.
Amesema kua watu wengi walimfikia wakimuomba atafute njia ya kusuluhisha mgogoro unaoendelea na ambao umesababisha vifo vya watu wengi kaskazini mwa Nigeria.
Aliongeza kusema kua ana idhini ya uongozi wa makundi yote pamoja na wakuu wa serikali ya Nigeria bkuanzisha mchakato wa amani.
Alisema pia kua Boko Haramu limeitaka serikali iwaandikie barua Boko Hamaramu kama mwaliko wa kushiriki mazungumzo yab amani.
Serikali ya Jimbo la Bauchi imekiri kua ilihusika katika juhudi za kuandaa mazungumzo hayo kwa niaba ya serikali kuu ya Nigeria.
No comments:
Post a Comment