TANGAZO


Sunday, May 27, 2012

Zanzibar hali tete


Mmoja wa waandamanaji wa Kundi la Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara  ya  Kiislamu (JUMIKI), kisiwani Unguja, akionesha kitambaa kilicho na damu mapema leo asubuhi, wakati wakiendelea na maandamano yao ambayo yamesababisha vurugu kubwa kisiwani humo, hali iliyosababisha kuchomwa moto kwa moja ya makanisa pamoja na baadhi ya magari yaliyokuwa yameegeshwa karibu na njia walizokuwa wakipita.

  Waandamanaji wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam (JUMIKI), wakiendelea na maandamano yao mapema leo asubuhi mjini Zanzibar.

Askari wa Jeshi la Polisi kikosi cha kutuliza ghasia (FFU), wakifanya doria katika mitaa mbalimbali ya mji wa Zanzibar mapema leo asubuhi.

No comments:

Post a Comment