TANGAZO


Sunday, May 27, 2012

Makamu wa Rais Dk. Bilal azindua vitabu vya Mzee Makamba

Katibu Mkuu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yussuf Makamba, akizungumza na wageni mbalimbali waliohudhuria katika uzinduzi wa vitabu vyake viwili alivyovitunga na kuzindualiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dk. Mohamed Gharib Bilal, ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam leo.  Vitabu vilivyozinduliwa ni pamoja na Binadamu na Kazi na Ukweli kwa Mujibu wa Biblia na Kuruani Tukufu, Suna za Mtume (SAW) na Sheria za nchi. (Picha zote na Kassim Mbarouk)


 Baadhi ya Wanazuoni wa Kiislamu waliokuwepo kwenye uzinduzi huo, wakifuatilia maelezo na hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa ukumbini hapo leo.


 Mchapishaji wa vitabu hivyo, Mbunge Nyangwina Nyambari, akizungumza kabla ya uzinduzi wa vitabu hivyo, ukumbini hapo.




  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza wakati alipokuwa akivizindua vitabu hivyo, ukumbini hapo leo asubuhi.


 Baadhi ya Wanazuoni na wageni mbalimbali waliohudhuria kwenye uzinduzi huo, wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi, Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, wakati alipokuwa akizungumza ukumbini hapo.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dk. Gharib Mohamed Bilal, akikata utepe uliofungiwa vitabu hivyo, wakati alipokuwa akikizindua moja ya vitabu viwili vilivyotungwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yussuf Makamba, anayemsaidia (kulia), Dar es Salaam leo. Kushoto anayesaidia ni mkewe, Josephine Makamba.


Makamu wa Rais, Dk. Gharib Mohamed Bilal, akinyanyua juu nakala za moja ya vitabu viwili vilivyotungwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yussuf Makamba (kulia), wakati akivizindua, Dar es Salaam leo. Kushoto mkewe, Josephine Makamba. Vitabu alivyovizindua Makamu wa Rais ni pamoja na Binadamu na Kazi na Ukweli kwa Mujibu wa Biblia na Kuruani Tukufu, Suna za Mtume (SAW) na Sheria za nchi.


Mke wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Luteni mstaafu, Yussuf Makamba, Josephine Makamba, akimpatia zawadi mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, wakati wa uzinduzi huo. 


 Baadhi ya akinamama, Wabunge na wageni mbalimbali waalikwa waliofika kwenye uzinduzi huo, wakifuatilia hotuba iliyokuwa ikitolewa na mgeni rasmi kwenye uzinduzi, Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal.


 Mtoto wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Luteni Yussuf Makamba, Mwamvita Makamba, akifurahia uzinduzi wa vitabu hivyo, vilivyotungwa na baba yake, Mzee Yussuf Makamba.


 Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya watu wa Iran, Morteza Sabourt (kushoto), akimkabidhi zawadi ya Msahafu wa Kuruan Tukufu maalum, mtuzi wa vitabu vya Binadamu na Kazi na Ukweli kwa Mujibu wa Biblia na Kuruani Tukufu, Suna za Mtume (SAW) na Sheria za nchi, Mzee Yussuf Makamba.

 aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yussuf Makamba (kulia), akiufunua Msahafu huo, aliopewa zawadi na Mkurugenzi huyo. Kushoto ni mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal.



 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita akimapatia zawadi, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho, Mzee Yussuf Makamba (kulia), wakati wa uzinduzi huo.


 Mwanazuoni wa Kiislamu, Seikh Ally Al Kharoos, akimkabidhi zawadi ya msahafu na mswala wa kuswalia, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yussuf Makamba, mara baada ya kuzinduliwa kwa vitabu vyake hivyo na Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Ghari Bilal (wa pili kulia), ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam.


 Mwanazuoni wa Kiislamu, Sheikh Ismail Mohamed Salim, akimpatia zawadi ya ubao wenye maandishi ya Kuran, mtunzi wa vitabu hivyo, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yussuf Makamba (kulia), mara baada ya kuzinduliwa na Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal (wa pili kulia), ukumbi wa Karimjee jijini leo. 


 Mtunzi wa vitabu vya Binadamu na Kazi na Ukweli kwa Mujibu wa Biblia na Kuruani Tukufu, Suna za Mtume (SAW) na Sheria za nchi, Katibu Mkuu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Luteni Yussuf Makamba, akikiangalia kifimbo alichopewa zawadi na mmoja wa marafiki zake, wakati wa uzinduzi huo. Kushoto ni mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal.

Katibu Mkuu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Luteni Yussuf Makamba (katikati), akizungumza na baadhi ya akinamama waliohudhuria uzinduzi huo, nje ya jengo la Karimjee, jijini Dar es Salaam leo.


Baadhi ya wanafamila ya Katibu Mkuu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Luteni Yussuf Makamba, wakiwa katika picha ya pamoja, mara baada ya uzinduzi wa vitabu hivyo, nje ya ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mke wake, Josephine Makamba na watatu kushoto ni mtoto wake Mwamvita Makamba.

No comments:

Post a Comment