TANGAZO


Sunday, May 27, 2012

Lagarde aambiwa amewatusi Wagiriki

Serikali ya Ufaransa imelalamika juu ya matamshi ya mkuu wa Shirika la Fedha Duniani, IMF, Christine Lagarde, ambayo yalionesha kuwa Wagiriki wanahepa kulipa kodi.

Christine Lagarde, mkuu wa IMF
Akihojiwa na gazeti moja la Uingereza, Bi Lagarde alisema Jumamosi, watu wa Ugiriki wakilipa kodi wanaweza kuisaidia nchi yao kujikwamua kutoka msukosuko wa kiuchumi.
Waziri mmoja wa Ufaransa, Najat Vallaud-Belkacem, alisema aliona matamshi hayo yanafanya tatizo la Ugiriki kuwa rahisi, na yanawatia Wagiriki wote kwenye fungu moja.
Mjini Athens, kiongozi wa chama cha kisoshalisti, Evangelos Venizelos, aliuambia mkutano wa kampeni za uchaguzi kwamba Bi Lagarde amewatusi wananchi wa Ugiriki.
Mkuu wa IMF piya alisema kwenye mahojiano hayo, kwamba ana wasiwasi zaidi juu ya umaskini katika nchi za Afrika kusini ya Sahara, kushinda Wagiriki waliokumbwa na msukosuko wa kiuchumi.

No comments:

Post a Comment