Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, akifafanua jambo mbele ya wageni mbalimbali waalikwa, waliofika kwenye mkutano uliohusu maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika.
Balozi Charles Stith, ambaye aliwahi kuwa balozi wa Marekani nchini Tanzania (Mratibu mkuu wa mkutano), akifafanua jambo kwa wageni waalikwa, wakati wa mkuatno huo.
Wageni mbalimbali waalikwa, waliofika kuhudhuri mkutano wa maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika, wakifuatilia mijadala mbalimbali iliyokuwa ikiendelea kabla ya kumalizika kwa mkutano huo, jijini humo jana.
Mmoja wa wageni waalikwa wa mkutano huo, akichangia jambo katika mkutano huo.
Wageni waalikwa wakifuatilia jambo wakati mkutano ukiendelea.
Wageni mbalimbali waalikwa, waliohudhuria mkutano wa kujadili maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika, Mkutano uliowakutanisha Marais wastaafu nane wa Afrika, umefikia tamati leo ndani ya Chuo Kikuu cha Witwatersrand, jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Tanzania, Ally Hassan Mwinyi, akiagana na Balozi Charles Stith, ambaye aliwahi kuwa balozi wa Marekani nchini Tanzania (Mratibu Mkuu wa Mkutano), mapema jana jioni, mara baada ya mkutano wa siku tatu uliojadili maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika na kuwakutanisha Marais Wastaafu nane wa Afrika, kufikia tamati jana.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Tanzania, Benjamin Mkapa, akiagana na Balozi Charles Stith, aliyewahi kuwa balozi wa Marekani nchini Tanzania, mapema jana jioni, mara baada ya mkutano wa siku tatu uliojadili maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika na kuwakutanisha Marais Wastaafu nane wa Afrika, kumalizika.
Rais Mtsaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, akiagana na Balozi Charles Stith ambaye aliwahi kuwa balozi wa Marekani nchini Tanzania (Mratibu mkuu wa mkutano), mapema jana jioni, mara baada ya mkutano wa siku tatu uliohusu kujadili maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika, kumalizika jana jioni.
Wahariri wa vyombo vya habari kutoka nchini Tanzania, wakiagana na Marais Wastaafu wa Tanzania, mara baada ya mkutano wa kujadili maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika, kumalizika ndani ya Chuo Kikuu cha Witwatersrand, jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
Rais Mstaafu, Nicéphore Dieudonné Soglo wa Benin, akiagana na Balozi Charles Stith ambaye aliwahi kuwa balozi wa Marekani nchini Tanzania (Mratibu mkuu wa mkutano), mapema jana jioni, mara baada ya mkutano wa siku tatu uliohusu kujadili maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika, kumalizika jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
Kushoto mstari wa mbele ni Balozi Charles Stith, aliyewahi kuwa balozi wa Marekani nchini Tanzania (Mratibu mkuu wa mkutano), Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi pamoja na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Abeid Aman Karume, wakiwa katika picha ya pamoja jana jioni na Wahariri wa vyombo vya habari kutoka Tanzania, mara baada kumalizika kwa mkutano wa kujadili maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika, jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
Baadhi ya Wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), wakiwa katika picha ya pamoja mapema jana, mara baada ya kushiriki mkutano wa kujadili maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika. Mkutano huo, uliowakutanisha Marais Wastaafu nane wa Afrika, umefikia tamati jana ndani ya Chuo Kikuu cha Witwatersrand, jijini Johannesburg, Afrika Kusini. (Picha na Ahmed Michuzi-Johanneburg)
No comments:
Post a Comment