Balozi wa Uganda nchini Uingereza, Mama Joan Rwabyomere, akifungua maadhimisho ya Siku ya Afrika nchini Uingereza, katika sherehe ambazo zilifanyika katika Ukumbi wa Hotel ya Lagham Palace, jijini London.
(Kwa hisani ya mdau Justina-george)
Balozi wa Botswana nchini Uingereza, Roy Blackbeard, akihutubia katika sherehe za kuadhimisha Siku ya Afrika.
Kutoka kulia, Rahma Lupatu, Caroline Chipeta, David Nginila, Kiondo (maafisa wa Ubalozi wa Tanzania, London) na Jestina George
Mabalozi, Maofisa wa Ubalozi na wawakilishi kutoka nchi mbalimbali za Afrika na wageni waalikwa wakiwa katika sherehe hizo.
Jestina George (kushoto) na Rahma Lupatu, wakijivunia Utanzania wao kwa kukunjua bendera ya Tanzania wakati wa sherehe hizo, za siku ya Afrika.
Kikundi cha ngoma kutoka Ghana, kikitoa burudani katika sherehe za kuadhimisha Siku ya Afrika jijini London jana.
No comments:
Post a Comment