TANGAZO


Tuesday, May 15, 2012

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Muhongo, Naibu wake, watembelea mitambo ya kuzalisha umeme, Ubungo, Dar es Salaam

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia), akisalimiana na wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Makao Makuu, Ubungo Dar es Salaam, wakati alipofika kwa ajili ya kukagua mitambo na kuangalia uzalishaji wa nishati hiyo leo. (Picha zote na mpigapicha wetu)

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, akisaini kitabu cha wageni alipofika Makao Makuu ya Tanesco, Ubungo jijini Dar es Salaam leo.


Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (wa tatu kulia), akipatiwa maelezo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Eng. William Mhando, wakati alipokuwa akitembelea moja ya mitambo ya kuzalishia nishati ya umeme, Ubungo jijini Dar es Salaam leo. Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Stephen Maselle.


Meneja wa Mitambo ya kuzalisha umeme wa Songas Ubungo, Ambaksye Mbangula (wa pili kulia), amkimpatia maelezo Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, kuhusu bomba la kupelekea gesi ya kuendeshea mitambo hiyo, linavyofanyakazi wakati alipotembelea mitambo hiyo leo, kujionea uzalishaji wa nishati hiyo.

Meneja wa Mitambo ya kuzalisha umeme wa Songas Ubungo, Ambaksye Mbangula (kulia), amkitembeza Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, sehemu zenye mitambo ya kuzalishia umeme, wakati alipotembelea mitambo hiyo, kujionea hali ya uzalishaji nishati hiyo, Dar es Salaam leo.


Meneja wa Kampuni ya mitambo ya kuzalisha umeme ya Symbion, Ubungo jijini Dar es Salaam, Moses Mwandenga (Plant Manager), kushoto, akitoa maelezo kwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa pili kushoto) na Naibu Mawaziri wake, George Simbachawene (wa kwanza kulia) na Stephen Maselle (wa pili kulia), wakati walipotembelea mitambo hiyo, kuangalia uzalisaji wa nishati hiyo leo.
Baadhi ya mitambo ya kuzalisha nishati ya umeme kwa kutumia gesi, iliyoko Ubungo, ambayo imetembelewa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na Naibu Mawaziri wake, George Simbachawene na Stephen Maselle, kuangalia maendeleo ya uzalishaji nishati hiyo.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) na Naibu Mawaziri wake, George Simbachawene na Stephen Maselle, wakipatiwa maelezo ya jinsi nishati ya umeme, inavyoingizwa kwenye Gridi ya Taifa na ugawaji wake, Makao Makuu ya Tanesco, Ubungo jijini Dar es Salaam, walipotembelea kuangalia maendeleo ya uzalishaji nishati hiyo kwenye mitambo ya Makampuni mbalimbali yanayozalisha nishati hiyo na kuingizwa kwenye Gridi ya Taifa.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (wa nne kulia), akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Makampuni ya kuzalisha umeme Ubungo pamoja na viongozi wa Tanesco, Ubungo mara baada ya kutembelea Makampuni hayo, kujionea shughuli za uzalishaji nishati hiyo leo asubuhi.

No comments:

Post a Comment