Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, akitoa hotuba yake wakati alipokuwa akizindua Kampeni ya 'STANDUP FOR AFRICAN
MOTHERS', iliyoandaliwa na AMREF ambapo aliwataka wananchi kutoa
ushirikiano wa kupunguza vifo vya akinamama wajawazito na watoto wao, wakati wa kujifungua. Mama Salma, alisema kuwa kila mwananchi akichangia
Sh.1000 za Kitanzania, zitasaidia kusomesha wakunga 4222, watakaotumika
kuwauguza akina mama wajawazito pindi wanapokuwa kwenye kipindi cha
kujifungua. Uzinduzi huo ulifanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam leo. (Picha na mpigapicha wetu)
Waziri wa Afya n Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi akitoa hotuba yake, wakati wa uzinduzi
huo, ambapo aliitaka Amref isaidie kukusanya pesa kutoka kwa nanchi
pamoja ana Makampuni binafsi ili fedha za kusomesha wakunga zipatikane.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Amref, wakisherehekea wakati wa uzinduzi huo.
Mama Salma Kikwete, akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Amref, Dk. Festus Ilako kwa kuonyesha upendo kwa akinamama wajawazito.
Kikundi cha burudani cha Mjomba Band, kikionesha mchezo wa sarakasi wakati wa uzinduzi huo, Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam leo.
No comments:
Post a Comment