Naibu Waziri Mkuu wa Uturuki, Bulent Arinc, akifungua mkutano wa Jukwaa la
Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki mjini Ankara, Uturuki wiki
iliyopita. Mkutano huo ulishirikisha wawakilishi wa vyombo vya habari na
wadau wengine kutoka nchi 54 za Afrika.
Mhariri Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, Willy Edward akiwasilisha mada katika mkutano wa Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki kuhusu 'Vyombo vya Habari kama kichocheo cha ushindi wa vita dhidi ya migogoro na ugaidi' mjini Ankara, Uturuki wiki iliyopita. Mkutano huo ulioandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, ulishirikisha wawakilishi wa vyombo vya habari na wadau wengine kutoka nchi 54 za Afrika.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia wakati Mhariri Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, Willy Edward (mbele kwenye skrini), akiwasilisha mada katika mkutano wa Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki, kuhusu 'Vyombo vya Habari kama kichocheo cha ushindi wa vita dhidi ya migogoro na ugaidi' mjini Ankara, Uturuki wiki iliyopita. Mkutano huo ulioandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Uturuki, ulishirikisha wawakilishi wa vyombo vya habari na wadau wengine kutoka nchi 54 za Afrika.
Mhariri wa Habari wa Gazeti la Nipashe Jumapili, Beatrice Bandawe(wa pili kushoto), akifuatilia mkutano wa Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki mjini Ankara, Uturuki wiki iliyopita.
Mkurugenzi wa Raia Mwema aliyepata pia kuwa MhaririMtendaji wa gazeti hilo na Kampuni ya New Habari Corporation 2006, John Bwire (kushoto) na Mhariri wa Makala wa Habari Leo, Selemani Nzaro wakifuatilia mkutano wa Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki mjini Ankara, Uturuki wiki iliyopita. Mkutano huo ulioandaliwa na ofisi ya
Waziri Mkuu Uturuki, ulishirikisha wawakilishi wa vyombo vya habari na wadau wengine kutoka nchi 54 za Afrika.
Mhariri Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, Willy Edward (kushoto), akipokea tuzo maalumu kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Jamhuri ya Uturuki (Idara ya Habari na Maelezo), Murat Karakaya iliyotolewa kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu Uturuki, Bulent Arinc, aliyemwakilisha Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Recep Tayyip Erdogan, baada ya kuwasilisha mada katika mkutano wa Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki kuhusu 'Vyombo vya Habari kama kichocheo cha ushindi wa vita dhidi ya migogoro na ugaidi' mjini Ankara, Uturuki wiki iliyopita. Mkutano huo ulioandaliwa na ofisi ya Waziri Mkuu, ulishirikisha wawakilishi wa vyombo vya habari na wadau wengine kutoka nchi 54 za Afrika.
Profesa Mohamed Bakari, raia wa Kenya anayefundisha Chuo Kikuu cha
Fatih nchini Uturuki, akipokea tuzo maalumu iliyotolewa kwa niaba ya
Naibu Waziri Mkuu Uturuki, Bulent Arinc baada ya kuwasilisha mada katika
mkutano wa Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki kuhusu 'Afrika
ya Leo: Sera za Siasa, Uchumi na Mambo ya Nje' mjini Ankara, Uturuki
wiki iliyopita. Mkutano huo ulishirikisha wawakilishi wa vyombo vya
habari na wadau wengine kutoka nchi 54 za Afrika.
No comments:
Post a Comment