Tuesday, May 15, 2012
Jambo Leo latunukiwa cheti cha kuthaminiwa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Kamishna Msaidizi (ACP), David Misiime (wa pili kulia), akimkabidhi cheti Mhariri wa Michezo wa Gazeti la Jambo Leo, Julius Kihampa ikiwa ni katika kuthamini mchango wa gazeti hilo katika kuripoti mchezo wa ngumu pamoja na pambano la Ubingwa wa IBF kati ya Francis Cheka na Mada Maugo. Hafla hiyo, imefanyika Dar es Salaam leo, ambapo Kampuni ya Kitwe General Traders ilitoa vyeti hivyo pia kwa vyombo vingine vya habari, ambavyo vilitumia muda wao, kuutangaza mchezo wa huo na hasa mchezo huo wa Ubingwa wa IBF Afrika, ambao Cheka alishinda kwa KO.
Kampuni ya Kitwe Traders ndiyo iliyoandaa pambano hilo la ubingwa wa Afrika ambapo iliahidi kuendelea pia kuandaa mapambano mengine makubwa katika mchezo huo. (Picha na Dotto Mwaibale)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment