TANGAZO


Tuesday, May 15, 2012

Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Shariff, akabidhi Kombe la Jihad Cup, Zanzibar


 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya  Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad, akikabidhi Kombe la ushindi la “Jihadi Cup” kwa Nahodha wa timu ya Sayari, iliyoibuka kidedea kwenye ligi hiyo, iliyozishirikisha timu 9 za daraja la Pili na tatu kwa Wilaya ya Mjini Zanzibar.

 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad, akisalimiana na wachezaji wakati alipokuwa akikagua timu ya Taifa Jipya, iliyoingia kwenye finali za Jihadi Cup, huko Uwanja wa Amaan, mjini Zanzibar. Taifa Jipya ilishindwa na wapinzani wao timu ya Sayari kwa mikwaju ya penalty 5-3.

 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Rais wa Serikali ya Zanzibar,  Maalim Seif Sharif Hamad, akikagua timu ya Sayari, iliyoingia kwenye finali za “Jihadi Cup”, huko Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar. Sayari ilinyakuwa ubingwa kwa kuwashinda wapinzani wao timu ya Taifa Jipya kwa mikwaju ya penalty 5-3.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Rais wa Serikali ya Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa katika picha ya pamoja na Mwakilishi wa Jimbo la Magogoni, Abdillahi Jihadi Hassan (kushoto kwake) pamoja na baadhi ya viongozi wa ZFA na Kamati ya michezo ya “Jihadi Cup”, wakati wa fainali hizo. (Picha na  Salmin Said-Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanziba)

No comments:

Post a Comment