Spika wa Bunge, Anne Makinda akiweka shada la maua katika eneo maalumu lililotengwa kwa ajili ya kumbukumbu ya wahanga wa mafuriko ya Tsunami, yaliyoikumba nchi ya Japan mwezi Machi mwaka jana, alipowasili nchini humo jana na kutembelea Mji wa NATORI, uliopo Mkoa wa MIAGA ikiwa ni mojawapo ya miji iliyokumbwa na mafuriko yaliyoikumba Japan. Spika na ujumbe wa wabunge 5, wapo katika ziara ya kikazi nchini humo kwa mwaliko maalumu wa Bunge la Japan. (Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge)
Spika wa Bunge, Anne Makinda akimkabidhi zawadi, Naibu Meya wa Mji wa Natori, Takamoto Ohta (kushoto) mara baada ya kufanya nae mazungumzo baada ya kuwasili katika mji huo kwa lengo la kujionea uharibifu ulitokana na mafuriko ya Tsunami yaliotokea Machi mwaka jana, ambapo zaidi ya watu 911 walipoteza maisha na wengine 53 kutopatikana mjini humo.
Spika wa Bunge, Anne Makinda akiwa katika mazungumzo maalumu na Naibu Meya wa Mji wa Natori, Takamoto Ohta (kushoto) mara baada ya kuwasili katika mji huo kwa lengo la kujionea uharibifu ulitokana na mafuriko ya Tsunami yaliotokea Machi mwaka jana, ambapo zaidi ya watu 911, walipoteza maisha na wengine 53 kutopatikana katika mji huo. Spika na ujumbe wake, wapo katika ziara nchini Japani kwa mwaliko maalumu wa Bunge la Japani.
Naibu Meya wa Mji wa Natori, Takamoto Ohta, akimuonesha katika ramani, Spika Makinda sehemu kubwa ya maeneo yalioathirika na mafuriko hayo katika Mji wa Natori.
Spika wa Bunge, Anne Makinda akiwa katika mazungumzo maalumu na Naibu Meya wa Mji wa Natori, Takamoto Ohta (kushoto), mara baada ya kuwasili katika mji huo kwa lengo la kujionea uharibifu ulitokana na mafuriko ya Tsunami yaliotokea mwezi Machi mwaka jana, ambapo zaidi ya watu 911 walipoteza maisha na wengine 53 kutopatikana.
Spika Nakinda, akiangalia baadhi ya mabaki ya wahanga wa Mfuriko hayo kwenye picha katika Shule ya Awali ya YORIAGE, ambapo picha na nguo za wanafunzi waliofariki zimehifadhiwa.
Spika akiangalia baadhi ya mabaki ya wahanga wa mafuriko hayo kwenye kwenye albamu ya picha katika Shule ya Awali ya YORIAGE, ambapo picha na nguo za wanafunzi waliofariki zimehifadhiwa.
Magari yalioharibika na mafuriko yakiendelea kuondolewa katika eneo hilo.
Baadhi ya mabaki ya meli, zilizosombwa na mafuriko hayo, zikiwa katika eneo la mji huo.
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Spika wa Tanzania, Anne Makinda (wa pili kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Meya wa Mji wa Natori, Takamoto Ohta (wa pili kulia), mara baada ya kuweka shada la maua katika eneo maalumu lililotengwa kwa ajili ya kumbukumbu ya wahanga wa mafuriko ya Tsunami, yaliyoikumba nchi ya Japan, Mwezi Machi mwaka jana, alipotembelea mji wa NATORI, uliopo Mkoa wa MIAGA, ikiwa ni mojawapo ya miji, iliyokumbwa na mafuriko yaliyoikumba Japani, mwaka jana. Spika Makinda na ujumbe wa Wabunge 5, wapo katika ziara nchini humo kwa mwaliko maalumu wa Bunge la Japan. Kushoto ni Tundu Lissu, Anne Makinda, Rukia Ahmed, James Lembeli, Anne Kilango Malecela, Naibu Meya wa Mji wa Natori, Takamoto Ohta na Godfrey Zambi.
Spika wa Bunge, Anne Makinda akiwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Narita, mjini Tokyo, kwa ziara ya siku 6 ya kikazi kwa mwaliko wa Bunge la Japani. Kulia ni kwake ni Balozi wa Tanzania nchini humo, Salome Sijaona. Spika katika ziara hiyo ameongozana na ujumbe wa Wabunge 5 kutoka Bunge la Tanzania.
No comments:
Post a Comment