TANGAZO


Tuesday, May 15, 2012

Mawaziri Profesa Tibaijuka, Dk.Theresia Huvisa wazungumza na waandishi

 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu uvamizi wa maeneo ya fukwe za bahari na ya mito, ambapo aliwataka wavamizi hao kuondoka ama kujitayarisha kuondolewa na kuongeza kuwa hata wale walioewa kihalali wataondolewa kwenye maeneo hayo,ya mita sitini kutoka baharini. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, Dk. Terezya Huvisa, aliyefuatana naye na kuzungumza na waandishi kwa pamoja. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, akiwaonesha waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, moja ya ramani zilizokosewa michoro yake na kusababisha kuchukuliwa kwa maeneo ya kiraia,maeneo ya Kazi Mzumbwi, Kisarawe, mkoani Pwani. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, Dk. Terezya Huvisa, aliyeshirikiana naye kwenye mkutano huo na waandishi wa habari, kuelezea ukiukwaji wa ujenzi wa mipango miji na kuharibiwa kwa mazingira ya miji na vijiji.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, akiwaonesha waandishi wa habari, ramani hiyo, Dar es Salaam leo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, Dk. Terezya Huvisa, akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano huo leo, kuelezea uharibifu wa mazingira ya maeneo mbalimbali kutokana na kutokufuatwa kwa taratibu za ujenzi wa mipango miji pamoja na ujenzi holela katika maeneo yaliyopimwa kutokana na baadhi ya wamiliki kujiongezea na kujipimia wenyewe maeneo hayo. Katikati ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, aliyefuatana naye na kushirikiana naye kuzungumza na waandishi wa habari jijini leo na Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari (Maelezo), Jamal Zuberi.

Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mazungumzo ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, Dk. Terezya Huvisa, walipozungumza nao kuhusu ukiukwaji wa sheria za mipango miji na uharibifu wa mazingira.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, Dk. Terezya Huvisa (kushoto) na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, wakiwaonesha waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, ramani zinazoonesha ujenzi holela katika eneo la Mto Ndumbwi, maeneo ya Kawe, ambalo sehemu ya mto huo imebanwa kutokana na mmiliki wa eneo karibu na mto huo  kujiongezea eneo na kujenga hadi sehemu ya mto huo, hivyo kusababisha uharibifu wa mazingira na pia kukiuka sheria za mipango miji.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, Dk. Terezya Huvisa, akiwaonesha waandishi wa habari sehemu ya mto huo, ilipobanwa kutokana na ujenzi usiofuata mipango miji iliyokuwepo tokea 2005. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Baraza la Mazingira  (NEMC), Dk. Robert Ntakamulenga na Kaimu Kamishna Msaidizi wa Ardhi (Sheria), Irene Godfrey.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, akisistiza jambo wakati alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari kwenye mkutano huo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari (Maelezo), Jamal Zuberi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, akiionesha ramani ya mto huo, uliofinywa kutokana ujenzi holela, wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari kwenye mkutano huo. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, Dk. Terezya Huvisa.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Baraza la Mazingira (NEMC), Dk. Robert Ntakamulenga, akitoa ufafanuzi kwa waandishi wakati walipokuwa wakiuliza maswali kuhusu sehemu mbalimbali zenye uharibifu wa mazingira hususan za viwanda na mito. Kushoto ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka na katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, Dk. Terezya Huvisa.

Baadhi ya waandishi wa habari wakinukuu maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mawaziri hao kwenye mkutano wao wa pamoja na waandishi wa habari, Idara ya Habari, Maelezo jijini Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment