TANGAZO


Thursday, May 10, 2012

Waziri Mwinyi afungua Kongamano la Siku ya Wauguzi, Muhimbili

Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Agnes Mtawa, akisoma majina ya wafanyakazi bora wa hospitali hiyo wakati wa maadhimisho ya Siku ya wauguzi,  ambapo Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi, alikuwa mgeni rasmi katika wa maadhimisho hayo, Dar es Salaam jana. (Picha zote na Khamisi Mussa)


 Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya taifa ya Muhimbili (MNH), wakiwa katika kongamano hilo, wakipiga makofi wakati Waziri Mwinyi akizungumza nao kwenye ufunguzi huo jana.



Waziri wa Afya na  Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi, akimvalisha nishani Dk. Skolastika Ndende wakati wa hafla hiyo.


Waziri wa Afya na  Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi, akimvisha nishani Sister Teddy Kurwa, wakati wa hafla hiyo.

Mkurugenzi wa Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk. Marina Njelekela, akimkabidhi tuzo Waziri wa Afya na  Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi, mara baada ya kulifungua kongamano la Siku ya Wauguzi, hospitalini hapo jana. 

Waziri wa Afya na  Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi, akimkabidhi tuzo Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Agnes Mtawa, wakati wa hafla hiyo.

 Waziri wa Afya na  Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi, akikiabidhiwa tuzo na Mwenyekiti wa Chama cha Wauguzi nchini (TANA), Paulo Magesa (kushoto) na Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini wa MNH, Profesa Joseph Kizilwa, wakati wa hafla hiyo.

 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi, akiagana na Madaktari mara baada ya kuzindua maadhimisho ya Siku ya Wauguzi duniani hospitalini hapo jana.


Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi, akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kuzindua maadhimisho ya Siku ya Wauguzi duniani hospitalini hapo.



 Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Agnes Mtawa (kushoto), Mkurugenzi wa Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk. Marina Njelekela (katikati), wakizungumza na Ofisa wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, Mama Kasanjala, wakati wa hafla hiyo.


Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi, akipiga picha ya kumbukumbu na baadhi ya wafanyakazi wa MNH, mara baada ya kufungua kongamano la maadhimisho ya Siku ya Wauguzi, hospitalini hapo jana.



 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi, akiagana na Mkurugenzi wa Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk. Marina Njelekela, mara baada ya kufungua kongamano hilo. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini wa MNH, Profesa Joseph Kizilwa.

No comments:

Post a Comment