TANGAZO


Thursday, May 10, 2012

Mapacha wa mdau Bayana blog, wapata ubatizo

Padre Mike Snyder, akimpaka mafuta mmoja wa watoto mapacha anayeitwa Collina Mrema, wakati wa hafla ya Ibada ya Ubatizo kwenye Kanisa Katoliki la Muhimbili, Dar es Salaam juzi. (Picha zote na Khamisi Mussa)



Padre Mike Snyder, akimbatiza pacha mwingine Collin Mrema, wakati wa hafla ya Ibada ya Ubatizo iliyofayika kwenye Kanisa Katoliki la Muhimbili, Dar es Salaam juzi. 



Padre Mike Snyder, akimbatiza kwa maji Collina Mrema, wakati wa hafla ya Ibada ya Ubatizo iliyofanyika kwenye Kanisa hilo. 



Padre Mike Snyder, akimpaka mafuta mtoto Collin Mrema, wakati wa hafla ya Ibada hiyo iliyofanyika kwenye Kanisa Katoliki la Muhimbili, Dar es Salaam juzi. 



Padre Mike Snyder, akimweka kitambaa cha kumwombea mambo mema mtoto Collin Mrema, wakati wa hafla ya Ibada hiyo kanisani juzi. 



Watoto mapacha Collin (kushoto) na Collina Mrema, wakiwa nje ya Kanisa hilo, mara baada ya Ubatizo Kanisani  hapo. 



Watoto mapacha Collin (kulia) na Collina Mrema, wakiwa na mama yao, Elizabeth Matilia, nje ya Kanisa hilo, mara baada ya Ibada ya Ubatizo Kanisani  hapo. 


Watoto mapacha Collin (kulia) akiwa na baba wa ubatizo, Dk. Tumaini Simon na Collina Mrema, wakiwa na mama wa ubatizo, Jane Evarist, nje ya Kanisa hilo, mara baada ya Ibada ya Ubatizo wao.



Watoto mapacha Collin na Collina Mrema, wakiwa na pamoja na familia na jamaa wa familia yao nje ya Kanisa hilo, baada ya Ibada ya ubatizo Kanisani  hapo. 



Wazazi wa watoto mapacha Collin na Collina Mrema, pamoja na marafiki wa familia hiyo, wakipata chakula nyumbani kwao baada ya shughuli ya ubatizo kukamilika na kurudi nyumbani.

No comments:

Post a Comment