TANGAZO


Wednesday, May 9, 2012

Rudisha atamani kushindana na Bolt

 

David Rudisha
David Rudisha
Bingwa wa dunia wa mbio za mita 800 ikiwa anatazamiwa kushinda medali ya dhahabu kwenye mashindano ya Olimpiki mjini London, David Rudisha, anasema ana tamaa ya kupambana na Usain Bolt katika mbio zinaostahili wote wawili.
Akizungumza mbele ya wandishiwa habari kabla ya mashindano ya Diamond League mjini Doha yatakayofanyika siku ya Ijumaa, Rudisha amesema ametafakari uwezekano wa kushindana na Bolt kwa mbio ambazo angeanza kwa kujiandaa ingawa haoni hilo likitimia.
Mkenya huyo alichagua mbio za mita 400 kupokezana vijiti kama mbio za kutimiza ndoto yake, ambapo wangechuana katika mbio ambazo wote wanazipenda.
Rudisha amesema kua ingembidi yeye ashuke kutoka mbio za mita 800 huku Bolt akipanda kutoka mbio zake za mita 100 na 200 kusawazisha uwezo wa kila mmoja.
Usain Bolt
Usain Bolt
Rudisha, hukimbia mbio za mita 400 kuzidisha kasi yake na amesema huko Doha kua Usain Bolt ana kasi, mimi sina kasi kama yake lakini nina kasi inayoniwezesha kwenda mwezo mrefu. Ndiyo sababu ingefurahisha kuona jinsi mwisho ungekuaje.
Rudisha, anashiriki mbio za Doha bila jeraha na anasema kua mbio hizi zitamsaidia kujinoa kwa ajili ya mashindano ya mjini London.
Kijana huyu mwenye umri wa miaka 23 amefanikiwa katika mbio hizi ingawa bado hajafanikiwa kushinda medali ya dhahabu, ameongezea kusema kua akiweza kuweka mda bora mjini Doha basi atajiona kua tayari na njiani kufanikisha ndoto ya kujishindia medali ya dhahabu.
Mjini Doha, hatokua na mpinzani mkali baada ya Mohammed Aman kujiondoa kwenye mashindano.
Kijana huyo kutoka Ethiopia mwenye umri wa miaka 18 alimshinda Rudisha kwenye mbio za mjini Milan mwezi Septemba mwaka jana mjini Milan na pia kwenye mashindano ya Dunia mnamo mwezi March mwaka huu.

No comments:

Post a Comment