TANGAZO


Tuesday, May 8, 2012

Waziri Fenella, Naibu wake waripoti ofisini


Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, akifurahi na baadhi ya watumishi, mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara hiyo, zilizopo katika jengo la Golden Jubilee, jijini Dar es Salaam leo. (Picha zote kwa Hisani ya WHVUM)




Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, akisaini katika kitabu cha wageni, mara baada ya kuwasali katika Ofisi za Wizara hiyo leo kuanza kazi. Anayeshuhudia ni Katibu Mkuu, Sethi Kamuhanda.


 Baadhi ya Watendaji wa Wizara na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, wakimsikiliza Waziri Dk. Fenella Mukangara, wakati alipokuwa akiongea na Uongozi wa Wizara hiyo. Kushoto ni Mhasibu Mkuu wa Wizara, Rose Bandisa, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Leornard Thadeo (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa TBC, Clement Mshana.


Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara, akisisitiza jambo kwa viongozi wa Wizara na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo, mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara hiyo. Kulia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Amos Makalla na kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara, Sethi Kamuhanda.



Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Amos Makalla akiongea na Uongozi wa Wizara hiyo, mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara leo asubuhi. 

No comments:

Post a Comment