TANGAZO


Tuesday, May 8, 2012

Rais wa Zanzibar afanya ziara ya kuimarisha Chama Kusini Unguja

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Dk. Ali Mohamed Shein, akifungua pazia kama ishara ya uwekaji wa jiwe la msingi, Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya  Wadi ya Koani,  Shehia ya  Kidimni, Wilaya ya Kati, Unguja leo, alipokuwa katika ziara ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi, Mkoa wa Kusini Unguja. (Picha na Ramadhan Othman, Ikulu)


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Dk. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi cheti cha utambulisho kwa wananchi wa jimbo la Koani kada wa CCM, Salmini Awadh, Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni, akiwa ni miongoni mwa  waliochangia kufanikisha matembezi ya mshikamano. Sherehe hizo zimefanyika leo Ofisi ya CCM Koani, Shehia ya Kidimni, Wilaya ya Kusini Unguja.


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ambaye  pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Dk. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi cheti cha utambulisho kwa wananchi wa jimbo la Koani, kada Naila Jidawi, akiwa ni miongoni mwa  waliochangia kufanikisha matembezi ya mshikamano wakati wa hafla hiyo.



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ambaye  pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na wananchi pamoja na wanachama wa CCM, Jimbo la Koani, katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la Ofisi ya Wadi ya Koani, Shehia ya Kidimni, Wilaya ya Kusini Unguja leo.

No comments:

Post a Comment