Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar, Dickson D,Kaganga, akimuonesha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud, maeneo yalioathirika zaidi baada ya Kanisa hilo, kuchomwa moto katika vurugu zilizotokea mjini Zanzibar juzi, ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa na baadhi yao kuhusishwa na tokeo hilo, wakati alipotembelea Kanisa hilo kujionea uharibifu uliofanywa kwenye shambulizi hilo.
(Picha na Yussuf Simai, Maelezo Zanzibar)
(Picha na Yussuf Simai, Maelezo Zanzibar)
Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohamed Aboud, akimueleza jambo Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar, Dickson D,Kaganga (wa kwanza kulia), kuhusiana na kuchomwa moto kwa Kanisa hilo, lililopo Kariakoo mjini Zanzibar. Katikati ni Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Saidi Mwema.
Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar, Dickson D,Kaganga akimueleza jambo Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohamed Aboud na Viongozi wengine mbalimbali, kile kilichotokea baada ya Kanisa hilo kuchomwa moto katika vurugu zilizotokea mjini Zanzibar ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa na baadhi yao kuhusishwa na tokeo hilo.
Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar, Dickson D,Kaganga akibubujikwa na machozi kwa kuguswa na hotuba iliyokuwa ikitolewa na Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohamed Aboud, baada ya Kanisa hilo kuchomwa moto katika vurugu zilizotokea mjini Zanzibar, ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa na baadhi yao kuhusishwa na tukio hilo.
Mkuu wa Dini ya Kiislam, Ofisi ya Mufti wa Zanzibar, Thabit Noman Jongo, akitoa hotuba ya Dini inavyoeleza kuhusiana na kudumisha Amani na Usalama katika nchi na kuondosha mifarakano na chuki na kutokuharibu mali, kwenye kanisa hilo, mjini Zanzibar, ambalo limechomwa moto.
Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Saidi Mwema akitoa hotuba kwa Maaskofu na baadhi ya waumini wa Kikristo katika Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar, lililochomwa moto, ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa na baadhi yao, kuhusishwa na tukio hilo. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini, Abdalla Mwinyi na kushoto kwake ni Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar, Abdalla Mwinyi Khamis, akitoa hotuba na kuonyesha umoja na mshikamano uliokuwepo kati ya Waislam na Wakristo kwa kuonesha picha ambayo imebuniwa na mchoraji wa Kingereza na kuwataka kuendelea na mshikamano wao ili kuzidi kuleta amani nchini.
No comments:
Post a Comment