TANGAZO


Tuesday, May 29, 2012

Idd Simba na wenzake 2, wafikishwa mahakamani Kisutu, Dar es Salaam


 Waziri wa zamani wa Viwanda na Biashara wa Serikali ya Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, aliyekuwa Mbunge wa Ilala na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), Idd Simba, akiongozwa na askari Polisi, wakati akitoka mahakamani baada ya kusomewa kesi yake iliyokuwa na mashtaka nane yanayohusu ubadhirifu wa fedha za shirika hilo, pamoja na wenzake watatu, Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam leo. 



 Waziri wa zamani wa Viwanda na Biashara wa Serikali ya Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, aliyekuwa Mbunge wa Ilala na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), Idd Simba, akitoka mahakamani baada ya kusomewa kesi yake iliyokuwa na mashtaka nane yanayohusu ubadhirifu wa fedha, kiasi cha sh. milioni 320 za shirika hilo pamoja na wenzake watatu, Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam leo. 


Idd Simba, akizungumza jambo na Wakili wake Said Hamad El-Maamry (kushoto), baada ya kuachiwa kwa dhamana na wenzake kwenye kesi hiyo, Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo. 

Mmoja wa watuhumiwa katika kesi hiyo, Aliyekuwa Diwani wa Sinza, Salum Mwaking'anda akiwa katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo mchana.

No comments:

Post a Comment