Mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa ya Walinzi wa Amani, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mahadhi Juma Maalim (kushoto), akiwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Kazi la Umoja wa Mataifa (ILO), Hopolang Phororo (katikati) na Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi nchini, Meja Jeneral Hassan Vuai Chema, wakati wa maadhimisho hayo, Mnazi Mmoja jijini leo.
Wageni pamoja na mabalozi mbalimbali wa nchi za nje nchini, wakiwa wamesimama kwa ajili ya kutoa heshima zao katika maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa ya Walinzi wa Amani, yaliyoadhimishwa kwenye Viwanja vya Mashujaa, Mnazi Mmoja, Dar es Salaam leo.
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa ya Walinzi wa Amani, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mahadhi Juma Maalim, akiweka shada la maua chini ya Mnara wa Mashujaa, Mnazi Mmoja leo, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa ya Walinzi wa Amani.
Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN), Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Kazi la Umoja wa Mataifa (ILO), Hopolang Phororo, akiweka shada la maua kwa ajili ya kuadhimisha siku hiyo jijini leo.
Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi nchini, Meja Jeneral Hassan Vuai Chema, akiweka shada la maua kwenye mnara wa Mashujaa, Viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa maadhimisho hayo jijini leo.
Baadhi ya wananchi wakiangalia kupitia kwenye seng'enge za uzio wa uwanja wa Mashujaa, matukio yaliyokuwa yakitendeka kwenye maadhimisho hayo, viwanjani hapo leo.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Azania, wakiimba wimbo unaoitwa 'Peace and Love, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa ya Walinzi wa Amani, Viwanja vya Mashujaa Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam leo Mei 29, 2012.
Baadhi ya wapiga picha wa vyombo mbalimbali vya habari, wakirekodi na kuchukua picha za matukio mbalimbali katika maadhimisho ya siku hiyo, viwanjani hapo.
Baadhi ya wanajeshi waliowahi kushiriki katika ulinzi wa amani kwenye nchi mbalimbali za Kiafrika, wakiwa kwenye maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa ya Walinzi wa Amani, viwanjani hapo leo.
Baadhi ya waambata wa Kijeshi wa Balozi mbalimbali za nje ya nchi waliopo nchini, wakiwa kwenye maadhimisho ya siku hiyo, viwanjani hapo leo.
Baadhi ya Mabalozi wa nchi mbalimbali za nje ya nchi, waliopo nchini, wakiwa kwenye maadhimisho ya siku hiyo, viwanjani hapo, wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakitendeka.
Kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kiwa kimetulia kusubiri amri ya kufanya kutoka kwa Kamanda wao, wakati wa maadhimisho hayo.
Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN), Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Kazi la Umoja wa Mataifa (ILO), Hopolang Phororo, akisoma hotuba yake wakati wa maadhimisho ya siku hiyo.
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa ya Walinzi wa Amani, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim, akisoma hotuba yake, kwenye maadhimisho ya siku hiyo, jijini leo.
Mwakilishi wa Ofis ya Umoja wa Mataifa (UN), kitengo cha Habari, akitoa shukurani kwa mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim, wananchi na wageni mbalimbali walioshiriki kwenye maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa ya Walinzi wa Amani, viwanjani hapo.
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa ya Walinzi wa Amani, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mahadhi Juma Maalim,
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa ya Walinzi wa Amani, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mahadhi Juma Maalim, akisalimiana na kuagana na mmoja wa askari Polisi, aliyewahi kwenda katika nchi za Kiafrika, kufanya kazi ya ulinzi wa Amani.
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa ya Walinzi wa Amani, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mahadhi Juma Maalim, akisalimiana na kuagana na mmoja wa askari wa kike wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), aliyewahi kwenda katika nchi za Kiafrika, kufanya kazi ya ulinzi wa Amani, wakati akiondoka kwenye viwanja vilivyofanyika maadhimisho hayo.
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa ya Walinzi wa Amani, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mahadhi Juma Maalim, akizungumza na waandishi wa habari waliokuwa wakifuatilia maadhimisho ya siku ya Umoja wa Mataifa ya Walinzi wa Amani nchini.
Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi nchini, Meja Jeneral Hassan Vuai Chema, akizungumza na waandishi wa habari waliokuwa wakifuatilia maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa ya Walinzi wa Amani nchini, jijini leo.
No comments:
Post a Comment