TANGAZO


Wednesday, May 9, 2012

Washindi wa droo ya pili ya Vumbua hazina chini ya kizibo, wapatiakana

Meneja wa Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Teddy Mapunda, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati wa kuchezeshwa droo ya pili ya promosheni ya Vumbua hazina chini ya kizibo, ambapo washindi wawili wa jenereta na mmpoja wa pikipiki, walipatiakana. Kulia ni Ofisa wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Bakar Maggid na kushoto ni Meneja bia ya  Premium Serengeti Lager, Allan Chonjo. (icha na Kassm Mbarouk)

  Meneja wa Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Teddy Mapunda, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati wa kuchezeshwa droo ya pili ya promosheni ya Vumbua hazina chini ya kizibo. Kushoto ni Tumamiel Malisa, Ofisa wa Kampuni ya Push Mobile na Meneja wa bia ya Premium Serengeti Lager, Allan Chonjo.

 Meneja wa bia ya Premium Serengeti Lager, Allan Chonjo, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati wa kuchezeshwa droo ya pili ya Vumbua hazina chini ya kizibo. Katikati ni  Meneja wa Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Teddy Mapunda na Kulia ni Ofisa wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Bakar Maggid, akifuatilia mchezo huo. 

Maofisa kutoka Kampuni ya Push Mobile, wakichanganya na kuzichezesha namba za simu za wateja wao walioshiriki katika promosheni ya Vumbua hazina chini ya kizibo, Dar es Salaam leo. Aliyesimama kushoto, mstari wa nyuma ni Ofisa wa michezo ya Kubahatisha nchini, Bakar Maggid,

 Wadau wa blogu hii, wakiangalia matukio ya picha mbalimbali ya watu yaliyoko kwenye blogu ya Bayana, wakati wa kuchezeshwa droo hiyo leo.

Maofisa kutoka Kampuni ya Push Mobile, wakichanganya na kuzichezesha namba za simu za wateja wao walioshiriki katika promosheni ya Vumbua hazina chini ya kizibo, Dar es Salaam leo. Aliyesimama kulia, mstari wa nyuma ni Ofisa wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Bakar Maggid, akifuatilia mchezo huo.
 Baadhi ya waandishi wa habari, wakifuatilia matokeo ya droo ya pili ya Vumbua hazina chini ya kizibo, wakati ilipokuwa ikichezeshwa kwa ajili ya kuwapata washindi wa majenereta mawili na pikipiki moja leo asubuhi.

 Meneja wa bia ya Premium Serengeti Lager, Allan Chonjo, akizungumza na mmoja wa washindi wa droo hiyo, jijini Dar es Salaam, wakati ilipochezeshwa Dar es Salaam leo.

Baadhi ya waandishi wa habari, wakifuatilia matokeo ya mchezo huo, wakati ukichezshwa na Maofisa wa Kampuni ya Push Mobile, Dar es Salaam leo asubuhi.

No comments:

Post a Comment