Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (katikati), alikifuatana na viongozi na kuingia katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA), Tunguu katika mkutano wa watendaji wa Ofisi za Serikali Mkoa wa Kusini Unguja, wakati wa mkutano wa majumuisho uliofanyika Chuoni hapo leo, baada ya kumalizikia kwa ziara ya Rais katika Mkoa huo. (Picha nzote na Ramadhan Othman,Ikulu)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na watendaji wa Ofisi za Serikali, Mkoa wa Kusini Unguja, katika mkutano wa majumuisho wa ziara yake, uliofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu leo, baada ya kumaliziki kwa ziara katika Mkoa huo.
Baadhi ya Viongozi na watendaji katika Ofisi mbalimbali za Mkoa wa Kusini Unguja, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, alipokuwa na mazungumzo na watendaji hao, katika mkutano wa majumuisho ya ziara yake, aliyoifanya katika Mkoa wa Kusini Unguja. Mkutano huo umefanyika leo katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu, Wilaya ya Kati Unguja.
No comments:
Post a Comment