Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (kushoto), akimtembeza Mwenyekiti wa Tume ya kukusanya maoni ya Katiba mpya, Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba kwenye Ofisi mpya ya Tume hiyo, iliyopo katika jengo jipya la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ghorofa ya kwanza. Makabidhiano hayo yalifanyika leo, wizarani hapo, jijini Dar es Salaam. Katikati ni Waziri wa Sheria na Katiba, Celina Kombani. (Picha na Mpigapicha wetu)
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (kushoto), akimueleza jambo Mwenyekiti wa Tume ya kukusanya maoni ya Katiba mpya, Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba, wakati wa makabidhiano ya Ofisi ya Tume hiyo, iliyopo katika jengo jipya la Wizara ya Mambo ya Ndani, ghorofa ya kwanza. Wa pili kushotoni ni Waziri wa Sheria na Katiba, Celina Kombani na Mbunge wa CCM, viti maalum Dar es Salaam, Angela Kairuki.
Mandhari ya Ofisi inavyoonekana kwa ndani.
Mwenyekiti wa Tume ya Kukusanya maoni ya Katiba mpya, Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Wariomba (wa tatu kulia), akiwa pamoja na viongozi wengine wa Tume hiyo, wakibadilishana mawazo kabla ya kuanza kwa hafla hiyo.
Baadhi ya wajumbe wa Tume ya Kukusanya maoni ya Katiba mpya, wakiingia kwenye ukumbi wa mikutano, tayari kwa kuanza kwa hafla ya makabidhiano ya Ofisi watakayoitumia.
Baadhi ya wajumbe wa Tume ya Kukusanya maoni ya Katiba mpya, wakitembea kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano wa jengo hilo, tayari kuanza kwa hafla ya makabidhiano ya ya Ofisi watakayoitumia.







No comments:
Post a Comment