TANGAZO


Wednesday, May 2, 2012

Dk. Mahanga wa CCM, ambwaga Mpendazoe wa Chadema Mahakamani Dar


Wananchi wakitoka nje ya Mahakama Kuu, Dar es Salaam leo, baada Fred Mpendazoe wa Chama cha Chadema, aliyefungua kesi ya kutaka kutenguliwa matokeo ya Ubunge wa Jimbo la Segerea, unaoshikiliwa na Dk. Makongoro Mahanga wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kushindwa katika kesi hiyo. (Picha zote na Kassim Mbarouk)


 Mlalamikaji katika kesi ya kutaka kutenguliwa matokeo ya Ubunge wa Jimbo la Segerea jijini, Fred Mpendazoe wa Chadema, akizungumza na waandishi wa habari, baada ya kushindwa katika kesi hiyo na mpizani wake Dk. Makongoro Mahanga wa CCM. 


 Wanachama na mashabiki wa CCM, wakiwa na bendera za chama hicho, wakishangilia ushindi wa Mbunge Makongoro Mahanga, alioupata Mahakama Kuu baada ya Mahakama hiyo, kuuthibitisha uhalali wa Ubunge wake katika kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa mpinzani wake, Fred Mpendazoe wa Chadema.




 Mbunge wa Jimbo la Segerea na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga, akiwapungia wanachama na mashabiki wa CCM, waliokuwepo Mahakama Kuu kusikiliza matokeo ya kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa Chadema katika Jimbo hilo, Fred Mpendazoe, baada ya Mahakama Kuu, kuuthibitisha uhalali wa ubunge wa Mbunge huyo leo.


 Mbunge wa Jimbo la Segerea na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga, akizungumza na waandishi wa habari, nje ya Mahama Kuu, jijini Dar es es Salaam, baada ya kushinda kesi ya kupinga Ubunge wake.

Mbunge wa Jimbo la Segerea na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga, akionesha dole gumba, kama ishara ya ushindi baada ya kumbwaga mpinzani wake, Fred Mpendazoe wa Chadema leo, Mahakama Kuu jijini.


Mbunge wa Jimbo la Segerea na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga, akipeana mkono na Wakili wake, Jerome Msemwa, baada ya kumbwaga mpizani wake, Fred Mpendazoe Mahakama Kuu katika kesi ya kupinga Ubunge wake. 


 Wanachama wa Chadema, wakionesha alama ya Chama hicho, nje ya Mahakama Kuu, na kuimba nyimbo za kudhihaki ushindi wa Mbunge wa Segerea na Naibu wa Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga, baada ya kumbwaga mpinzani wake, Fred Mpendazoe wa Chadema, aliyefungua kesi ya kupinga Ubunge wake.


Wanachama na mashabiki wa CCM na wa Chadema, wakisigana, wakati wa kushangilia ushindi katika kesi ya kupinga Ubunge wa Dk. Makongoro Mahanga dhidi ya Fred Mpendazoe wa Chadema, huku askari Polisi wakiwa makini kulinda amani, na utulivu nje ya Mahakama hiyo.


 Wanachama na mashabiki wa CCM na wa Chadema, wakipambana kwa maneno wakati wa kushangilia ushindi katika kesi ya kupinga Ubunge wa Dk. Makongoro Mahanga dhidi ya Fred Mpendazoe wa Chadema.

 Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, ambaye pia ni Mbunge wa Segerea, Dk. Makongoro Mahanga, akitoka Mahakama Kuu na gari lake baada ya Mahakama hiyo, kuuthibitisha ubunge wake baada ya kuitengua kesi iliyokuwa imefunguliwa na aliyekuwa mpinzani wake, Fred Mpendazoe wa Chadema.


 Askari Polisi wakiwa katika harakati za kuweka hali ya utulivu, baada ya makundi mawili ya wafuasi wa Vyama vya CCM na Chadema, kusigana katika kushagilia ushindi wa Ubunge wa Dk. Mahanga baada ya kumbwaga Mpendazoe wa Chadema, katika kesi aliyoifungua kupinga Ubunge wake, Mahakama Kuu jijini.


 Wanachama na mashabiki wa CCM, wakishangilia ushindi wa Dk. Mahanga, maeneo ya barabara ya City Drive, dhidi ya Mpendazoe wa Chadema,  katika kesi aliyoifungua Mahakama Kuu, kupiga Ubunge wake.


 Umati wa mashabiki wa CCM, ukiwa katika sherehe ya kushangilia ushindi wa kesi ya kupinga matokeo ya Ubunge wa Dk. Makongoro Mahanga, iliyofunguliwa na mpinzani wake, Fred Mpendazoe wa Chadema leo. 


Askari Polisi wakifuatilia msafara wa wanachama wa Vyama vya CCM na Chadema, uliokuwa ukishangilia na kutupiana maneno baada ya Mbunge wa Segerea, Dk. Makongoro Mahanga kumbwaga mpinzani wake, Fred Mpendazoe katika kesi aliyoifungua Mahakama Kuu kupinga Ubunge wake.


 Baadhi ya wanachama wa CCM, waliotoka Buguruni jijini Dar es Salaam. wakiondoka kwa shangwe kushangilia ushindi huo wa Mbunge wao, Dk. Makongoro Mahanga, Mahakama Kuu, jijini leo. 


Alieyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu nchini (FAT), Alhaj Ally Hassan Mwanakatwe, akiwapungia mashabiki na Wanachama wa CCM, waliokuwa wakishangilia ushindi wa Mbunge wa Jimbo la Segerea, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Makongoro Mahanga.


 Wapiga ngoma wakiongoza sherehe za ushindi wa Mbunge wa Jimbo la Segerea, Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga katika kesi iliyofunguliwa na mpinzani wake, Fred Mpendazoe wa Chadema, Mahakama Kuu, jijini.


 Mmoja wa mashabiki wa Mbunge Mahanga, akipeperusha bendera ya CCM, kwenye mtaa wa Azikiwe ulikopita msafara wa wafuasi na mashabiki wa Chama hicho.


Polisi wakiwa na gari lao, wakifuatilia msafara huo, ili kulinda amani kutokana na kusigana kwa wafuasi wa Vyama vya CCM na Chadema baada ya kutolewa huku ya kupiga Ubunge wa Dk. Mahanga, Naibu Waziri wa Kazi na Ajira leo mchana. 

No comments:

Post a Comment