TANGAZO


Saturday, May 26, 2012

Stars, Malawi hakuna mbabe

 Mchezaji wa timu ya Taifa (Taifa Stars), Haruna Moshi 'Boban', akijaribu kuwatoka wachezaji wa Malawi James Sangala (5) na Limbikani Mzava (12), wakati timu hizo zilipomenyana, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni na kumalizika kwa suluhu ya bila kufungana. (Picha zote na Kassim Mbarouk)


 Mbwana Samatta wa Stars (kulia), akipambana na James Sangala wa Malawi katika mchezo huo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni.


 Mwinyi Kazimoto wa Stars (kulia), akijaribu kumtoka James Sangala wa Malawi katika mchezo huo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.

Mchezji Haruna Moshi 'Boban' wa Stars (kulia), akijaribu kumtoka James Sangala wa Malawi katika mchezo huo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni.

 Mbwana Samatta wa Stars (kulia), akitafuta mbinu ya kumtoka Limbikani Mzava wa Malawi, wakati wa mchezo huo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.


Mwinyi Kazimoto wa Stars (kulia), akipambana James Sangala wa Malawi katika mchezo huo, Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam leo.


Haruna Moshi 'Boban' wa Stars (kulia), akizuiwa Limbikani Mzava wa Malawi katika mchezo huo,  uliochezwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam leo jioni.


 Mbwana Samatta wa Stars (kushoto), akikimbia na mpira kuelekea langoni kwa Malawi huku Chimango Kayira wa Malawi, akijaribu kutaka kumzuia, wakati wa mchezo huo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.

 Haruna Moshi 'Boban' wa Stars (kulia), akiuzuiya mpira huku akifuatwa na Limbikani Mzava wa Malawi katika mchezo huo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni.

 Kocha wa timu ya Taifa Stars, Kim Poulsen, akimweleza jambo kapteni wake, golikipa Juma Kaseja, mara baada ya kumalizika mchezo huo, Uwanja wa Taifa na timu hizo kutoka suluhu ya bila kufungana.


Kocha wa timu ya Taifa Stars, Kim Poulsen, akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo leo jioni. Kushoto ni Kocha wa Malawi, Kinnah Phiri.

No comments:

Post a Comment