Shirika la Fedha Duniani, IMF, linasema kuwa msukosuko katika eneo linalotumia sarafu ya euro, haukuelekea utaathiri vibaya nchi za Afrika, ambazo sarafu zao zinaelemea juu ya euro.
Naibu mkurugenzi wa IMF kuhusu Afrika, Roger Nord, ameiambia BBC kwamba bado anataraji uchumi wa mataifa ya Afrika, kusini ya Sahara, utakuwa kwa asili-mia-5.5.
Alisema IMF inatumai nchi za Afrika Magharibi, koloni za zamani za Ufaransa, zinazotumia CFA franc, zitakuwa kichumi kwa asili-mia-6.5, kwa sababu uchumi wa Ivory Coast umekua sana.
Bwana Nord alisema nchi za Afrika kusini ya Sahara, zimetanua uhusiano wa kibiashara miaka ya karibuni, na asili-mia-20 tu ya bidhaa zao zinakwenda Umoja wa Ulaya.
No comments:
Post a Comment