Mmoja wa wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), akionesha vidole viwili, ambayo ni alama ya Chama hicho, huku akiwa ameshika bango lenye ujumbe wa kukikandia Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakati wa mkutano wa Chama hicho, uliofanyika Viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam leo.
Wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wakionesha mabango yenye ujumbe mbalimbali, wakati wa mkutano wa Chama hicho, uliofanyika Viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam leo.
|
Mbunge wa Jimbo la Ubungo kupitia Chadema, John Mnyika, akiwasili kwenye Viwanja vya Jangwani kwa ajili ya mkutano wa hadhara wa Chama hicho leo. |
Wafuasi wa CHADEMA wakiwa wamejishika vichwa, wakati wa mkutano wa Chama hicho, Viwanja vya Jangwani, Dar es salaam leo.
Mewenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, akiwapungia wanachama wa Chama wakati alipokuwa akiingia Viwanja vya Jangwani kwa ajili ya mkutano wa hadhara jijini leo.
Baadhi ya viongozi wakuu wa Chama hicho, wakiwa kwenye jukwa kuu, wakati wa mkutano wa Chama jijini Dar es Salaam leo.
Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi 'Mr II, Sugu', akizungumza kwenye mkutano huo, viwanjani hapo leo. |
Wafuasi wa Chadema wakionesha vidole viwili pacha, alama inayotumiwa na Chama hicho, wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyijaka Viwanja vya jangwani, Dar es salaam leo. |
Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika, akizungumza katika mkutano huo, uliofanyika Viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam leo.
Mewenyekiti wa Taifa wa CHDEMA, Freeman Mbowe, akiwahutubia wafuasi wa chama hicho, leo katika Viwanja vya Jangwani, jijini Dar es salaam, wakati wa uzinduzi wa kampeni yao ya VUA GAMBA VAA GWANDA ambayo itazunguka mikoa yote ya nchini. (Picha zote na Dotto Mwaibale)
No comments:
Post a Comment