TANGAZO


Saturday, May 26, 2012

Nape afanya ziara mkoani Kagera


Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),  Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akimsalimia Mwenyekiti wa Chama Cha Walemavu, Wilaya ya Misenyi, mkoani Kagera, Simon Andrea, baada ya kufungua Baraza la Vijana wa CCM, Wilaya hiyo jana, May 25, Uwanja wa Mashujaa, wilayani humo. Waliosimama ni baadhi ya viongozi wa CCM na UVCCM walioshiriki ufunguzi huo.

Nape akiwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Kagera, Avelyne Mushi baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Bukoba, kuanza ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Kagera jana.

Nape akizungumza na viongozi Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Ofisi ya CCM Mkoa wa Kagera jana.

Nape akitoa salam za Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kwenye msiba wa mtumishi wa siku nyingi wa Serikali,  Balozi, Dk. Vedasto Kyaruzi, mjini Bukoba, baada ya kwenda kwenye msiba huo wakati wa kuaga mwili wa marehemu, tayari kwa mazishi yaliyofanyika jana mjini Bukoba.

Nape akikata utepe kuingia kwenye kambi ya Baraza la Umoja wa Vijana wa CCM, Wilaya ya Missenyi, mkoani Kagera, kwa ajili ya kufungua Baraza hilo.

Vijana wa CCM, waliopiga kambi hiyo ya Baraza la Vijana, Missenyi, wakimsikiliza Nape, wakati alipokuwa akiwahutubia mjini humo jana.

Nape  Nnauye, akimkabidhi cheti Kamanda wa Vijana wa CCM Mkoa wa Kagera, Dioniz Malinzi kwa kuwa mmoja wa waliowezesha kambi hiyo ya Baraza la Vijana kufanyika.

Baadhi ya viongozi kwenye kambi hiyo, wakimpungia mkono Nape wakati alipokuwa akiondoka kambini hapo.

No comments:

Post a Comment