Spika Makinda awa mgeni rasmi maadhimisho Siku ya Albino Lindi
Spika wa Bunge, Anne Makinda (Mb), akipata maelezo kutoka kwa Abdalah Omar kutoka Chama cha Albino Tanzania, juu ya matumizi ya mafuta maalum ya ngozi kwa ajili ya watu wenye ulemevu wa ngozi (albino), wakati alipotembelea mabanda ya maonesho ya bidhaa na huduma mbalimbali za watu wenye ulemavu wa Ngozi. Spika alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya saba ya siku ya Albino yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Lindi leo. (Picha zote na Owen Mwandumbya wa Bunge)
Spika wa Bunge, Anne Makinda (Mb), akipokea DVD maalumu kuhusu Albino na Maisha yao kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la Kiserikali la Under the Same Sun, Vicky Mtetema, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Albino yaliyofanyika Lindi. Shirika hilo ni mdau mkubwa wa watu wenye ulemavu wa ngozi na linajishughulisha na kutoa elimu kwa watu wenye ulemavu wa ngozi pamoja na kutoa misaada mbalimbali.
Dk. Mashingo Lerise kutoka Taasisi ya Magonjwa ya Ngozi na Saratani (Ocean Road), akimweleza Spika wa Bunge, Anne Makinda (Mb), juu ya huduma mbalimbali zitolewazo na taasisi hiyo kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino), baada ya Spika Makinda, kutembelea banda lao, wakati wa kilele cha Siku ya Albino Kitaifa, iliyofanyika Lindi leo. Kulia ni baadhi ya Madaktari wa Saratani ya ngozi kutoka taasisi hiyo, kutoka Hospitali za KCMC na Mkoani Lindi.
Spika akioneshwa mojawapo ya mafuta maalumu ya kuzuia Mionzi ya jua ambayo hutolewa bure na Serikali kupitia tassisi ya magonjwa ya ngozi kwa watu wenye ulemavu wa Ngozi.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzila, Spika wa Bunge, Anne Makinda, Mweneyikiti wa Chama cha Albino Tanzania, Ernest Kimaya na Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Danford Makala, wakipokea maandamano wakati wa kuadhimisha Siku ya Albino, mkoani Lindi leo, ambapo Spika alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya saba ya siku ya Albino yaliyofanyika kitaifa mkoani humo.
Waandamanaji wakipita mbele ya mgeni rasmi, Spika wa Bunge, Anna Makinda wakati wa maadhimisho ya Siku ya Albino leo.
Msanii Zakia Matimbwa, kutoka Albino Revolution Cultural Troup cha Dar es Salaam, akighani Ngonjera iliyobeba ujumbe wa kulaani mauji ya Albino wakati wa maadhimisho ya Saba ya Siku ya Albino, yaliyofanyika Kitaifa, mkoani Lindi leo.
Spika wa Bunge, Anne Makinda akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Lindi wakati wa maadhimisho ya Saba ya Siku ya Albino, yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Lindi leo.
Spika wa Bunge, Anne Makinda akisisitiza jambo wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Lindi wakati wa maadhimisho hayo ya saba ya siku ya Albino yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Lindi leo.
Wabunge Al Shymar Kwegir na Salum Barwan, wakiwa katika hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment