TANGAZO


Saturday, May 5, 2012

Rais Shein azindua jengo la Bima Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo la Makao Makuu ya Shirika la Bima Zanzibar, liliojengwa na Kampuni ya RANS COMPANY LIMITED. Uzinduzi huo, umefanyika leo Mpirani, mjini Zanzibar. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji na Mwenyekiti ya Bodi ya Wakandarasi Zanzibar, 'Zanzibar Contractors Association'  (ZACA), Nassor Khamis Al-Miskry. (Picha zote na Ramadhan Othman, Ikulu)

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Ali Mohamed Shein, akifungua pazia kama ishara ya uzinduzi wa Jengo la Makao Makuu ya Shirika la Bima Zanzibar, lililojengwa na Kampuni  ya RANS COMPANY LIMITED. Uzinduzi huo umefanyika leo, Mpirani mjini Zanzibar. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakandarasi Zanzibar, Nassor Khamis Al-Miskry.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akipata maelezo kutoka kwa Msimamizi wa ujenzi wa Kampuni ya RANS COMPANY LIMITED Nassor Khamis Al-Miskry ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakandarasi Zanzibar (ZACA), wakati alipolikagua Jengo la Makao Makuu ya Shirika la Bima Zanzibar baada ya kulizindua rasmi leo.

Wananchi waliohudhuria katika sherehe za uzinduzi wa Jengo jipya la Makao Makuu la Shirika la Bima Zanzibar, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, alipokuwa akizungumza baada ya uzinduzi rasmi wa jengo hilo leo, lililopo Mpirani, mjini Unguja.



Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Bima Zanzibar,  wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk .Ali Mohamed Shein, alipokuwa akiwahutubia, wakati wa uzinduzi wa Jengo jipya la Makao Makuu ya Shirika la Bima Zanzibar, Mpirani mjini Unguja leo.

No comments:

Post a Comment