TANGAZO


Saturday, May 5, 2012

Mama Kikwete azindua Uresco Saccos Mikocheni Dar es Salaam


  Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, akijumuika kucheza ngoma ya Sindimba iliyokuwa ikichezwa na akinamama, wakati wa sherehe ya uzinduzi wa Uresco saccos, huko Mikocheni A, jijini Dar es Salaam leo, tarehe 5.5.2012.
 
Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Uresco Saccos katika sherehe zilizofanyika katika Ofisi za Saccos hiyo, zilizoko Mikocheni jijini Dar es Salaam. Mama Salma ni mmoja wa wanachama wa saccos hiyo. Kushoto kwake ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mwantumu Mahiza.


Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete, akiwahutubia wanachama wa Uresco Saccos na wananchi waliohudhuria sherehe za uzinduzi rasmi wa Saccos hiyo, Mikocheni jijini leo.


Baadhi ya wanachama wa Uresco Saccos, wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi, Mama Salma Kikwete wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa Saccos yao, huko Mikocheni jijini Dar es Salaam leo. 

No comments:

Post a Comment