TANGAZO


Saturday, May 5, 2012

Mama Salma Kikwete, wake wa Makamu wa Rais watembelea Kambi ya Taifa Queens


Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, akitoa maelekezo kwa wachezaji wa timu ya Taifa ya Netiboli, 'Taifa Queens', wakati walipokuwa wakifanya mazoezi kwenye kambi yao, iliyoko katika Shule ya Sekondari ya Philbert Bayi, Kibaha wakati alipowatembelea jana, tarehe 4. 5. 2012. (Picha zote na John Lukuwi)

Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, akiangalia mazoezi ya timu ya Taifa ya Netboli, huko Kibaha mkoani Pwani jana kambini kwao.
 

Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, akiwaonesha mfano wachezaji wa timu ya Taifa ya Netboli, wakati alipofika kwenye kambi yao  jana.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, akiwapa somo la kucheza na kufunga magoli wachezaji wa Taifa Queens, wakati alipowatembelea kwenye kambi yao ya mazoezi, wakijiandaa kwa michuano ya Afrika itakayofanyika hapa nchini hivi karibuni.


Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete, akimkabidhi mchango wa shilingi milioni kumi, Mwenyekiti wa CHANETA, Anna Bayi, kwa ajili ya maandalizi ya timu ya Taifa ya mchezo huo. Makabidhiano hayo yalifanyika huko Kibaha jana kwenye kambi hiyo. 

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete, akifuatana na wake wa Makamu wa Rais, Zakhia (wa pili) na Asha Bilali (wa mwisho), wakiagana na wachezaji wa timu ya Taifa ya Netiboli huko Kibaha tarehe jana mara baada ya kuwatembelea na kufanya nao mazungumzo ya kuwapa hamasa.  

No comments:

Post a Comment