Spika wa Bunge, Anne Makinda,
akizungumza na Ujumbe wa Bunge la Sudan Kusini,
ulipomtembelea ofisini kwake Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni
Spika wa Bunge la Sudan Kusini, James Wani Igga, ambaye
ndiye kiongozi wa ujumbe huo, Henry Dilah Odwao, Mwenyekiti wa
Kamati ya Nishati na Madini, Mary Atong Bak, Makamu Mwenyekiti wa
Kamati ya Mambo ya Habari na Utamaduni, Dk. Kuong Dak Wie na Prof. George Bureng Nyumbe, wote kutoka Bunge la Sudan Kusini. (Picha zote na Owen David)
Spika wa Bunge, Anne Makinda, akimuonesha zawadi ya saa ya ukutani, yenye picha ya jengo la Bunge, Spika wa Bunge la Sudan Kusini, James Wani Igga, wakati ujumbe wa Wabunge wa Sudan Kusini ukiongozwa na Spika huyo, ulipomtembelea Spika Makinda ofisini kwake jijini Dar es salaam leo.
Spika wa Bunge, Anne Makinda, akimkabidhi zawadi ya saa ya ukutani yenye picha ya jengo la Bunge, Spika wa Bunge la Sudan Kusini, James Wani Igga, wakati yeye na ujumbe wake wa Wabunge kutoka Sudan Kusini ulipomtembelea
Spika, ofisini kwake, Dar es salaam leo. Wengine katika picha ni
wabunge hao, kutoka Sudan Kusini.
No comments:
Post a Comment