Moto wa mwenge utakaotumiwa
kuwasha mwenge wa mashindano ya Olimpiki mjini London uliwashwa mahali
yalipozaliwa mashindano ya kale ya Olimpiki siku ya Alhamisi.
Kukiwa na jua la kutosha angani, hapakua na sababu ya kutegemea moto kutoka kwingine wakati wa kufanya majaribio ya mwisho kuasha mwenge wa Olimpiki siku moja kabla.
Gianniotis ni mmoja wa watu 490 watakaotembeza mwenge huo mwendo wenye umbali wa kilomita 2,900 kupitia Ugiriki kabla haujakabidhiwa kwa watayarishaji wa mashindano ya London tareh 17 Mayyy.
Tafauti na tabia ya mashindano ya awali, ambapo mwenge huu unazungushwa dunia nzima, safari hii utavuka nje ya visiwa vya Uingereza mara moja u, kupitia Dublin mnamo tareh 6 Juni.
Mashindano ya Olimpiki yataanza tareh 27 Julai hadi tareh 12 Agosti 2012.
No comments:
Post a Comment