TANGAZO


Thursday, May 10, 2012

Ombudsman ahofia maisha yake Burundi


Mkuu wa uchunguzi wa malalamiko(Ombudsman) nchini Burundi, Mohamed Rukara, amegundua njama ya kumuua, kwa mujibu wa msemaji wake.
Mvutano upo Burundi
Mauwaji yazidi Burundi
"ni hao wanaoiba fedha za umma," amesema Jerome Ndiho, bila kutaja majina.
Kama mchunguzi huru,Bw.Rukara hufanya upelelezi juu ya madai yoyote yanayofanywa na maofisa wa serikali, ikiwa ni pamoja na ''njama za mauwaji ya raia''.
Makundi ya nchini humo yanadai kua serikali ya Burundi inawakinga watu wanaoshiriki rushwa na imeshindwa kukabiliana na ghasia zinazochochewa kisiasa.
'vitisho vya kuua'
Burundi bado inapitia kipindi cha ukarabati wake kifikra na kitaifa kufuatia vita vya miaka 12 ya wenyewe iliyomalizika mwaka 2005 -kisha ghasia za kisiasa zikafuata kufuatia uchaguzi ambao haukuridhisha baadhi ya raia mwaka 2010.
Kundi la kupigania haki APRODH, limeandika mauwaji yasiyopungua 160 mwaka huu, yanayolaumiwa kufanywa na makundi ya wanausalam.
Viongozi wakubaliana
Viongozi wakubaliana
Mapema mwezi huu, ripoti ya kundi la Human Rights Watch ilidokezea kila ilichokielezea kua 'kulipiza kisasi'' kwa watu waliosababisha mgawanyiko wa kisiasa kutoka pande zote mbili.
Bwana Rukara amesema kua endapo watauawa, ameomba asizikwe hadi Madaktari waifanyie uchunguzi maiti yake kuhakikisha kilichosababisha kifo chake.
Shirika lenye makao yake mjini New York, huma rights watch, linadai kua lilikataliwa kufanya makutano wa wandishi wa habari mjini Bujumbura kuhusu ripoti yao.
Hata hivyo wakuu wa nchi wamejibu madai hayo kama uzushi uliokithiri na kulaumu mauwaji juu ya makundi ya majangili wenye silaha.
Bw.Rukara aliteuliwa kama mchunguzi(ombudsman) wa kwanza nchini humo mapema mnamo mwaka 2011 kufuatia uteuzi uliofanywa na bunge- takriban miaka kumi baada ya bunge hilo kuundwa chini ya mapatano ya kwanza ya amani.
Inakadiriwa kua vita vya wenyewe kwa wenyewe baina ya makabila ya Watutsi na Wahutu nchini Burundi viomesababisha vifo vya hadi watu 30,000
Mzozo huo ulimalizika rasmi mwaka 2005 kwa mapatano ya amani yaliyofuatiwa na kuchaguliwa kwa Bw.Pierre Nkurunziza kama Rais wa nchi hio.
Kundi la mwisho la waasi lilisalimu amri mnamo mwaka 2009 lakini mashambulizi ya hapa na pale yanazidi kutokea na kusababisha baadhi ya raia wa nchi hio kukimbilia uhamishoni.

No comments:

Post a Comment