TANGAZO


Sunday, May 27, 2012

Simba watembeza Kombe la Ubingwa mitaani


 Wachezaji wa Simba wakiwa katika gari la wazi wakipita katika mitaa mbalimbali jijini Dar es Salaam leo, kulitembeza kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom, Tanzania Bara, kabla ya kuelekea kwenye ukumbi wa Der Live, Mbagala  kwa sherehe kabambe za ubingwa huo, walioutwaa hivi karibuni. (Picha zote na Dande Junior)

 Msafara wa mashabiki wa Simba ukipita katika mitaa ya Magomeni Mapipa, Dar es Salaam leo, ukizunguka kwenye mitaa mbalimbali ya jiji.

  Mashabiki na wapenzi wa Simba wakizunguka na Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom, mitaani ikiwa ni shamra shamra za sherehe kabambe ambayo itahitimishwa kwenye ukumbi wa Dar Live, Mbagala jijini Dar es Salaam leo.

Shabiki wa Simba akiwa amebeba picha kubwa ya mnyama Simba.

No comments:

Post a Comment