TANGAZO


Sunday, May 27, 2012

Redd's Miss Kurasini 2012, alivyopatikana

Wanenguaji wa bendi ya FM Academia, wakizirudi ngoma za kundi hilo, ukumbi wa Equator Grill, Mtoni Temeke, Dar es Salaam, wakati wa kumtafuta Redd's Miss Kurasini 2012, juzi usiku. (Picha zote na Dotto Mwaibele)


Warembo wakicheza ili kuonesha vipaji vyao katika kuzirudi ngoma, kabla ya kuaza kutembea katika mitindo mbalimbali ya kimadaha kwenye mchuano huo.



Warembo wakicheza ngoma kwa mitindo mbalimbali katika kuonesha vipaji vyao vya kuzirudi ngoma hizo, wakati wa mchuano huo.



Warembo wa Chamg'ombe, Temeke wakisalimia jukwa wakati walipofika kwenye ukumbi huo, kuangalia kinyang'anyiro cha Redd's Miss Kurasini 2012, Equator Grill juzi. 



Warembo wa Tabata, wakisalimia jukwa wakati walipofika kwenye ukumbi huo, kuangalia kinyang'anyiro cha Redd's Miss Kurasini 2012, Equator Grill juzi. 



Warembo, Angela Gasper (kushoto) na Irene Sosthen, wakipozi wakati walipokuwa wakionesha vazi laufukweni.




Flavian Maeda (kushoto) na Edina Magige, wakipozi na vazi la ufukweni katika kinyanganyiro hicho.



Lilian Joseph (kushoto) na Grace Blessing Kibona, wakipozi na vazi hilo.



Flavian Maeda (kushoto) na Edina Magige, wakipozi na vazi la ufukweni katika kinyanganyiro hicho.




Christina Moses (kushoto) na Mariam Sadik, wakipozi na vazi la ufukweni


Malikia wa mipasho, Khadija Kopa akiwapeleka puta mashabiki wa mipasho waliohudhuria kwenye kinyanganyiro cha mnyange wa Kurasini juzi usiku.


Mrembo Irene Sosthen, akipozi na vazi la kubuni wakati alipokuwa akitembea kuonesha mbwembwe zake na madaha ya kutembea kwenye jukwaa la kumsaka mnyange huyo.


Grace Blessing Kibona, akipozi na vazi la kutokea wakati wa kinyanganyiro hicho ukumbini hapo juzi usiki.


Flavian Maeda, akipozi na kuonesha vazi lake la kutokea wakati alipokuwa akionesha madoido na mbwembwe zake za kulitawala jukwa katika kinyang'anyiro hicho.


Jenifer Njabiri, akionesha vazi lake la kutokea kwenye kinyanganyiro hicho, ukumbini hapo juzi.


Christina Moses, akipozi na vazi lake la kutokea, wakati alipokuwa akitembea na kuonesha madaha yake kwenye kinyanganyiro hicho.


Mrembo Edina Magige, akitembea na vazi lake la kutokea kwenye jukwaa hilo, wakati wa kumsaka mlimbwende wa Redd's Miss Kurasini 2012, Equator Grill, Mtoni jijini juzi usiku.


Lilian Joseph, akipozi na vazi la kutokea kwenye kinyang'anyiro hicho, ukumbini hapo juzi usiku.


Mrembo Linda Nancy Joseph, akipozi na vazi lake la kutokea kwenye kinyanganyiro hicho, ukumbini hapo juzi usiku.


Baadhi ya warembo wa kinyanganyiro cha kumsaka Redd's Miss Kurasini 2012, wakiwa wamepozi wakisubiri kutajwa kwa matokeo ya wanyange walioingia kwenye tano bora.

Wanyange walioingia kwenye tano bora wakisubiri kwa hatua nyingine ya kuulizwa maswali na kujibu ili kuweza kumpata mshindi wa Redd's Miss Kurasini 2012.


Muandaaji wa mnyange wa Redd's Miss Kurasini 2012,  Mkurugenzi wa ZUM Fashion, Zuwena Mustafa, akimkabidhi Mkurugenzi wa PJ, Juma Mhina tuzo ya kuthamini mchango wake katika kufanikisha kupatikana mlimbwende wa Redd's Miss Kurasini 2012.



Muandaaji wa mnyange wa Redd's Miss Kurasini 2012,  Mkurugenzi wa ZUM Fashion, Zuwena Mustafa, akimkabidhi tuzo ya kuthamini mchango wa kufanikisha kupatikana mlimbwende wa Redd's Miss Kurasini 2012 kwa mmoja wa wadhamini wa kinyang'anyiro hicho.



Muandaaji wa mnyange wa Redd's Miss Kurasini 2012,  Mkurugenzi wa ZUM Fashion, Zuwena Mustafa, akimkabidhi Mhariri Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, Willy Edward, tuzo ya kuthamini mchango gazeti hilo katika kufanikisha kupatikana mlimbwende wa Redd's Miss Kurasini 2012.


Miss Kurasini 2011, Mwajabu Juma akimvisha mkanda wa Umiss Kurasini 2012, Flavian Maeda, mara baada ya kutangazwa mshindi wa kinyang'anyiro hicho.


Washindi watano wa kinyanganyiro hicho,  Elizabeth Peter wa 4 (kushoto), Lilian Joseph wa 3, (wa pili kulia),  Neema Doreen wa 2 (wa pili kushoto) na Agela Gasper wa 5 (kulia), wakiwa na Redd's Miss Kurasini 2012,  Flavian Maeda, wakipozi kwa picha mara baada ya kutangazwa kwa matokeo ya kinyang'anyiro hicho juzi usiku.


 Redd's Miss Kurasini 2012,  Flavian Maeda, akipozi na mshindi wa pili Neema Doreen (kushoto) na wa tatu, Lilian Joseph.



 Mshindi wa Redd's Miss Kurasini 2012,  Flavian Maeda (katikati), akitabasamu katika pozi na mshindi wa pili Neema Doreen (kushoto) na mshindi wa tatu, Lilian Joseph (kulia), mara baada ya kuvikwa mataji yao ukumbini hapo juzi usiku. 

No comments:

Post a Comment