TANGAZO


Sunday, May 27, 2012

Wakuu wa Mikoa, Wilaya watembelea Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) leo

Baadhi ya Michoro iliyochorwa na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), ikiwa kwenye moja ya chumba cha kuhifadhia kazi hizo. 

Baadhi ya Michoro ilichorwa na baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM), ambazo leo wamepata nafasi ya kuonyesha kazi zao tofauti na masomo wanayosomea.

Baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Wilaya, wakiwasili katika ukumbi wa Chimwaga uliopo Chuoni  hapo,. wakati wa maonyesho ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma yanayoendelea.


 Baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Wilaya wakisalimiana na wenyeji wao wakati walipofika  kwenye maonyesho ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma ambapo wanafunzi waliweza kuonyesha uwezo wao tofauti na masomo wanayosomea.

Mmoja wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM), akitoa maelezo kwa baadhi ya Wakuu wa Wilaya na Mikoa waliofika kuona kazi za wanafunzi wa UDOM wakati wanafunzi hao, wakionesha uwezo tofauti na masomo wanayosomea.

Wakuu wa Mikoa na Wilaya, wakitembelea jengo la Utawala la Chuo Kikuu Cha Dodoma na kufanya ziara ndani ya Chuo Kikuu Cha Dodoma, wakati walipofika Chuoni hapo kuangalia maonesho ya wanafunzi yanayoendelea katika ukumbi wa Chimwaga, Chuo Kikuu Cha Dodoma.

Baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Wilaya wakitembelea jengo jipya la Utawala la Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) leo.

 Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM), Mipango, Utawala na Fedha, Profesa Shaaban Mlacha (katikati), akitoa maelezo kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya waliotembelea Chuo hicho katika maonesho yaliyohusisha wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma.


 Wakuu wa Mikoa na Wilaya, wakiwa katika picha ya pamoja, mbele ya jengo jipya la Utawala, chuoni hapo leo. (Picha zote na Josephat wa Lukazablogspot)

-- 

No comments:

Post a Comment