Wanafunzi wa Shule ya Maandalizi ya Fujoni, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, alipokuwa akizungumza na wazee pamoja na watoto hao, baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule hiyo leo, akiwa katika ziara ya kuangalia maendeleo katika sekta mbalimbali za jamii, Wilaya ya Kaskazini B, Unguja.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Mbunge wa Jimbo la Kitope, Balozi Seif Ali Iddi, akiwasalimia wananchi wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la Shule ya Maandalizi ya Fujoni, lililowekwa na mgani rasmi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika ziara ya kuangalia maendeleo katika sekta mbalimbali za jamii, Wilaya ya Kaskazini B, Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akimsalimia mtoto Abdulsalami Omaar wa Fujoni, wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa Shule ya Maandalizi ya Fujoni, Jimbo la Kitope, alipokuwa katika ziara ya kuangalia maendeleo katika Wilaya ya Kaskazini B, Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa Shule ya Sekondari ya Kitope, Wilaya ya Kaskazini B, alipokuwa katika ziara ya kuangalia maendeleo katika sekta mbalimbali za kijamii katika Wilaya hiyo, Mkoa wa Kaskazini, Unguja leo. Kushoto ni Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Mbunge wa Jimbo la Kitope, Balozi Seif Ali Iddi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akifuatana na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kitope, Suleiman Juma Makame, wakati alipokuwa akikagua madawati katika madarasa ya mapya ya Shule hiyo leo, baada ya kuizindua rasmi, akiwa katika ziara ya kuangalia maendeleo katika sekta mbalimbali za kijamii Wilaya ya Kaskazini B, Unguja.
Wanafunzi wa Shule ya Kitope, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, wakati alipokuwa akizungumza na wazee katika sherehe za uzinduzi wa madarasa mapya ya Shule hiyo, baada ya uzinduzi leo, katika ziara yake ya kuangalia maendeleo katika sekta mbalimbali za kijamii, Wilaya ya Kaskazini B, Unguja.
Wanafunzi wa Shule ya Kitope, wakiga makofi kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, wakati alipokuwa akizungumza na wazee katika sherehe za uzinduzi wa madarasa mapya ya Shule hiyo, baada ya uzinduzi leo, katika ziara yake ya Wilaya ya Kaskazini B, Unguja leo.

No comments:
Post a Comment