TANGAZO


Thursday, May 3, 2012

Rais Kikwete, awateua Ubunge Janeth Mbene, James Mbatia, Profesa Muhongo



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amefanya uteuzi wa wabunge watatu wapya kwa mujibu wa Mamlaka ya Uteuzi aliyonayo chini ya Ibara ya 66 (i) (e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wabunge hao wapya ni Profesa Sospeter Muhongo, Bi. Janet Mbene na Bwana James Mbatia. Uteuzi huo unaanza mara moja.

Imetolewa na: Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Dar es Salaam, Mei, 2012



Mbunge Mteule, Bi. Janeth Mbene, aliyeteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kwa mujibu wa uwezo aliopewa na Katiba ya nchi katika nafasi zake 10 za uteuzi.


Mbuge mteule, Profesa Sospeter Muhongo
Rais Jakaya Kikwete akiwa na Mwenyekiti wa  Chama cha NCCR-MAGEUZI, James Mbatia, alipofika Ikulu jijini Dar es salaam Januari 22, 2012, kuwasilisha mapendekezo ya Chama chake, kuhusu mchakato wa Katiba mpya. Rais Kikwete leo, amewateua Mwenyekiti  Mbatia, Bi. Janeth Mbene na Profesa Sospeter Muhongo, kuwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment