Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,walioshiriki katika ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,wakisikiliza kwa Makini taarifa ya Mkoa wa Kusini Unguja iliyosomwa na Afisa Tawala wa Mkoa Sabri Mohamed.
Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Kusini, Unguja wakiwa katika mkutano wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, alipoanza ziara yake mkoani humo leo na kupata taarifa katika Ofisi ya Mkoa huo, huko Tunguu, Wilaya ya Kati Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein,(kushoto), akipokea taarifa ya kazi za utekelezaji wa Mkoa wa Kusini Unguja, kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Mkoa huo, Abdalla Mwinyi Khamis, leo alipoanza ziara yake na kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani humo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Ali Mohamed Shein (kulia), akipata maelezo kutoka wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamadunu na Michezo, Ali Mwinyikai, alipotembela eneo jipya linalojengwa Mnara wa Redio wa kurushia matangazo huko Bungi, Wilaya ya Kati Unguja,alipokuwa katika ziara ya Mkoa wa Kusini leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein,(katikati) na ujumbe, aliofuatana nao, wakitoka kuangalia mnara wa Redio ulioanza kufungwa na Kampuni ya Ujenzi ya Minara ya New Techinical Contractors Company ya Dar es Salaam, chini ya Injinia Stivin Makange (mwenye tai), huko Bungi Wilaya ya Kati Unguja leo, akiwa katika ziara ya Mkoa wa Kusini.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akifungua pazia kama ishara ya uwekaji wa jiwe la msingi wa nyumba ya Madakatari katika kituo cha Afya cha Unguja Ukuu leo, alipokuwa katika ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo katika Mkoa wa Kusini Unguja, iliyoanza leo, katika Wilaya ya Kati Unguja.

No comments:
Post a Comment