TANGAZO


Monday, May 7, 2012

Spika Makinda awasili Kigali kuhudhuria mkutano wa Maspika Afrika Mashariki

 Spika wa Bunge, Anne Makinda akiwasili katika Uwanja wa ndege wa Kigali baada ya
kupokelewa na Mwenyeji wake Spika wa Bunge la Rwanda, Rose Mukantabana (Kushoto). Makinda yupo Kigali Rwanda kuhudhuria Mkutano wa Saba wa Maspika wa Mabunge wananchama wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika leo.
 

 Spika Anna Makinda na Mwenyeji wake, Spika wa Bunge la Rwanda, Rose Mukantabana, wakiondoka Uwanja wa ndege mara baada ya Kuwasili.
 

 Spika wa Bunge, Anne Makinda akizungumza na Mwenyeji wake, Spika wa Bunge la Rwanda, Rose Mukantabana mara baada ya Kuwasili mjini Kigali kuhudhuria Mkutano wa Saba wa Maspika wa Mabunge wa Nchi wananchama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika leo.

Spika wa Bunge, Anne Makinda akipata maelezo  ya awali kuhusu Mkutano huo kutoka kwa maafisa wa Bunge la Tanzania. Wa kwanza Kushoto ni Justina Shauri , Afisa Dawati wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Bunge la Tanzania na Charles Mloka, Mkurugenzi wa Kamati za Bunge anayemuwakilisha Katibu wa Bunge katika Mkutano huo. (Picha na Owen Mwandumbya)

No comments:

Post a Comment