TANGAZO


Monday, May 7, 2012

Rais Kikwete, awaapisha Mawaziri, Ikulu jijini Dar es Salaam


Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, akiwasili katika viwanja vya Ikulu leo asubuhi kwa ajili ya kuwaapisha Mawaziri wapya aliowateua Ijumaa iliyopiita. (Picha na John Bukuku)
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akizungumza jambo na Katibu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, kabla ya kuanza kuapishwa kwa Mawaziri hao.
Rais Jakaya Kikwete, akimwapisha Dk. Harrison Mwakyembe kuwa Waziri wa Uchukuzi Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Shamsi Vuai Nahodha, akiapa mbele ya Rais Jakaya Kiwete kuwa mwaminifu katika kazi yake ya Uwaziri wa Ulinzi, Viwanja vya Ikulu jijini leo asubuhi. 
Dk. Husein Mwinyi akila kiapo cha uaminifu na utiifu katika kazi yake ya Uwaziri wa Afya na Ustawi wa Jamii mbele ya Rais Jakaya Kikwete katika hafla hiyo leo asubuhi.

Profesa Jumanne Maghembe, akisaini kiapo cha utiifu na uaminifu mara baada ya kuapa kuwa mbele ya Rais Jakaya Kikwete, aliyemteu katika nafasi ya Uwaziri wa  Maji na Umwagiliaji.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia akila kiapo cha utiifu na uaminifu katika kazi yake hiyo leo asubuhi, mbele ya Rais Jakaya Kikwete, aliyemteu tena kushika nafasi hiyo juzi, Ijumaa.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe, akikabidhiwa vitendea kazi na Rais Jakaya Kikwete mara baada ya kumwapisha kwenye viwanja vya Ikulu, leo asubuhi. 
Waziri wa Utawala Bora, George Mkuchika, akipongezwa na Rasi Jakaya Kikwete mara baada ya kumwapisha kuwa Waziri wa Wizara hiyo leo asubuhi, Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.



Waziri mpya wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Emmanuel Nchimbi, akila kiapo cha utii na uaminifu katika wadhifa wake huo, mbele ya Rais Jakaya Kikwete, kwenye Viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Richard Mwaikenda)

Mbunge wa Mvomero, Amos Makalla, akiapa mbele ya Rais Jakaya Kikwete, kuwa mtiifu na mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano na Rais wake, katika kutekeleza majukumu yake ya Unaibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, viwanjani hapo leo asubuhi.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akizungumza jambo na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) na Waziri mpya wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chizza (katikati), wakati wa hafla hiyo.

Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akimpongeza Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene, wakati wa hafla ya kuwaapisha Mawaziri na Naibu, Viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam.

Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja (kushoto), akimpongeza January Makamba ambaye ni Naibu Waziri wa Sayansi,Teknolojia na Mawasiliano, katikati wa hafla hiyo.

Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene, akiteta na Naibu Waziri wa Nisharti na Madini, Steven Masele, mara baada ya kula kiapo cha utii na uaminifu kwa Jumhuri na Rais Jakaya Kikwete.

Rais Jakaya Kikwete (mstari wa mbele katikati), Makamu wa Rais, Dk. Bilal (kulia kwake) na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (kushoto kwake), wakiwa katika picha hiyo na Mawazi na Naibu Mawaziri, mara baada ya kuwaapisha.

Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais, Dk. Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakiwa katika picha ya pamoja na Mawazi na Naibu Mawaziri, mara baada ya kuwaapisha leo asubuhi kwenye Viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam.

Rais Jakaya Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri walioapishwa leo asubuhi katika Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais Jakaya Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Mawaziri waliowaapisha leo asubuhi katika Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment