TANGAZO


Wednesday, May 30, 2012

Rais Kiwete amkaribishwa Rais Ouattara wa Ivory Coast nchini, azungumza naye

Rais Jakaya Mrisho Kikwete (wa pili kulia) na mgeni wake, Rais Allasane Ouattara (wa pili kushoto) wa Ivory Coast, wakitembea kwa miguu kuelekea sehemu waliyotengewa kufanyia mazungumzo rasmi, hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha leo, May 30, 2012 ambako Rais huyo wa amefika kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa  Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), ambao unafunguliwa rasmi kesho na Rais Kikwete katika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC), jijini humo. Katika maongezi yao, Rais Kikwete amesema Tanzania inaunga mkono juhudi za Ivory Coast za kutaka kurejeshwa nchini humo, Makao Makuu ya  AfDB, ambayo yamehamia Tunisia, kutokana na vurugu zilizotokea Abidjan baada ya Uchaguzi Mkuu mwaka jana.


Rais Jakaya Kikwete na Rais  Allasane Ouattara  wa Ivory Coast, wakiangalia shamba la kahawa wakati wakielekea sehemu waliyotengewa kufanyia mazungumzo yao, hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha leo May 30, 2012, ambako Rais huyo wa Ivory Coast amefika kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa AfDB, unaofunguliwa na Rais Kikwete kesho, ukumbi wa AICC. 


Rais Jakaya Kikwete (kulia) na mgeni wake, Rais Allasane Ouattara  wa Ivory Coast wakiangalia shamba la kahawa wakati wakielekea kabla ya kuelekea sehemu waliyotengewa kufanyia mazungumzo yao, hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha, ambako Rais huyo wa Ivory Coast amefika kuhudhuria mkutano wa AfDB, unaofunguliwa kesho na Rais Kikwete katika ukumbi wa AICC. 


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Allasane Ouattara wa Ivory Coast, wakiwa katika mazungumzo hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha leo May 30, 2012, ambako Rais huyo wa Ivory Coast amefika kuhudhuria mkutano wa AfDB, unaofunguliwa kesho na Rais Kikwete ukumbi wa AICC jijini humo. 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais  Allasane Ouattara  wa Ivory Coast, wakiagana baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao, hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha leo May 30, 2012, ambako Rais huyo wa Ivory Coast amefika kuhudhuria mkutano wa AfDB, unaofunguliwa kesho na Rais Kikwete kwenye ukumbi wa AICC. (Picha na Ikulu)

No comments:

Post a Comment