TANGAZO


Wednesday, May 30, 2012

Dk. Bilal amkaribisha Makamu wa Rais wa Iran nchini, azungumza naye

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal,
akimkaribisha Makamu wa Rais wa Iran, Mohammad Reza Rahimi, wakati alipowasili
ofisini kwake, Ikulu jijini Dar es Salaam kwa mazungumzo leo Mei 30, 2012. Makamu wa Rais wa Iran amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu. 


 Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa Iran, Mohammad Reza Rahimi, wakati alipofika ofisini kwake, Ikulu jijini Dar es Salaam kwa mazungumzo. Makamu huyo, amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu. Kulia ni Waziri wa Kazi wa Iran, Sheykhales Lam.

 Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Makamu wa Rais wa Iran, Mohammad Reza Rahimi, baada ya kumaliza mazungumzo yao, yaliyofanyika ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Mei 30, 2012. Kulia ni Waziri wa Kazi wa Iran, Sheykhales Lam na kushoto ni Mkalimaniwa wake. Makamu huyo, amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.

 Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Makamu wa Rais wa Iran,  Mohammad Reza Rahimi, baada ya kumaliza mazungumzo yao, yaliyofanyika ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam leo, Mei 30, 2012. Makamu wa Rais wa Iran yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.

 Makamu wa Rais wa Iran, Mohammad Reza Rahimi, akiweka saini katika kitabu cha
ofisi ya Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipofika ofisini hapo kwa mazungumzo leo. Kulia ni Waziri wa Kazi wa Iran, Sheykhales Lam. 

 Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Makamu wa Rais wa Iran, Mohammad Reza Rahimi, wakati alipofika ofisini kwake, Ikulu jijini Dar es Salaam leo kwa mazungumzo. Makamu wa Rais wa Iran amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.

Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Makamu wa Rais wa Iran,  Mohammad Reza Rahimi, baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao, yaliyofanyika ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam leo.  Makamu wa Rais wa Iran amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.

Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal (kushoto) na Makamu wa Rais wa Iran (kulia), Mohammad Reza Rahimi, wakiwa katika mazungumzo maalum, ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro, Dar es Salaam leo Mei 30, 2012. Makamu wa Rais wa Iran amewasili nchini kwa  ziara ya kikazi ya siku tatu.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim, akizungumza wakati wa hafla ya mazungumzo kati ya ujumbe wa Tanzania, uliokuwa ukiongozwa na Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal na wa Iran, uliokuwa chini ya Makamu wa Rais wa nchi hiyo, Mohammad Reza Rahimi, ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam leo Mei 30, 2012. Ujumbe huo, upo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu. (Picha zote na Muhidin Sufiani-OMR)

No comments:

Post a Comment