Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa (kushoto), akibadilishana hati ya mkataba wa mkopo nafuu na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Waarabu, inayojishughulisha na Maendeleo ya Uchumi wa Afrika (BADEA), Abdelaziz Khelef, jijini Arusha leo kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilometa 22.1, kutoka Wete hadi Chakechake, kisiwani Pemba. Mradi huo utagharimu shilingi bilioni 15.
Naibu Waziri wa Fedha, Saada Salum (katikakati), akibadilishana mawazo na Msemaji wa Wizara ya Fedha, Ingiahedi Mduma (kushoto), wakati wa mapumziko baada ya mikutano mbalimabli inayoendelea ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), jijini Arusha. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango ya Zanzibar, Amina Khamis Shaaban.
Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa, akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari jijini leo, mara baada ya kubadilishana hati ya mkataba wa mkopo nafuu na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Waarabu, inayojishughulisha na Maendeleo ya Uchumi ya Afrika (BADEA), Abdelaziz Khelef (kulia) kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilometa 22.1 kutoka Wete hadi Chakechake, kisiwani Pemba. Mradi utakao gharimu shilingi bilioni 15.
Waziri wa Fedha na Mipango, Ofisi ya Rais wa Serikali ya Zanzibar, Yusuf Omar Mzee, akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari leo jijini Arusha kuhusu umuhimu wa barabara mpya inayotarajiwa kujengwa kutoka Chake Chake hadi Wete kisiwani Pemba, mara baada ya Tanzania na Benki ya Waarabu inayojishughulisha na Maendeleo ya Uchumi wa Afrika (BADEA), kusaini mkataba wa mkopo wa masharti nafuu wa mradi wa ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilometa 22.1. Kulia ni Waziri wa Miundombinu, Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Zanzibar Hamad Masoud. (Picha zote na Richard mwangulube arusha)
No comments:
Post a Comment